
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe, amesema bado hawana mgombea wa urais ndani
ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),kwa vile wanaendelea
kuweka utaratibu mzuri zaidi wa kushiriksha kwa wanachama wao ili
kumpata mtu mwenye sifa na kukubalika kwa wananchi wote katika kuwania kugombea urais wa mwaka 2015.
Hivyo amesema , wakati ukifika mtu
yotote kutoka ndani ya umoja wao bila kujali wadhifa wake watakuwa na
fursa ya kujitokeza kuwania nafasi hiyo na atakayeonekana anafaa na kukubalika kutokana na sifa, uadilifu na uzalendo ataombwa atangulie mbele.
Mwenyekiti
huyo wa Taifa wa Chadema alisema hayo juzi , wakati akiwahutubia mamia
ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro ambao ukiwa ni mkutano wake mwisho baada ya kuzunguka mikoa mbalimbali nchini na kijiti kumkabidhi Katibu Mkuu wake kuendeleza ziara hizo.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kuwa, ushirikiano wa vyama
hivyo vinne si wa viongozi pekee badi ni vya wanachama na wananchi kwa
ujumla wao ambao wanakiu ya kupata mabadiriko .
“ Kilio cha ushirikiano huu si cha Mbowe au Lipumba na viongozi wengine wa Ukawa na
hatuendi na Ukawa ili kugawana vyeo , bali ni kuweka msingi wa
kumsimamisha mwenye uwezo na wengi wakimkubali...ataambiwa atangulie
mbele kuwaongoza watanzania wenzake” alisema Mbowe.
Pamoja na kusema, Ukawa haipo kwa misingi ya kugawana
vyeo, alisema upo kwa ajili ya kujenga nchi na hata walipo nje ya umoja
wao na hata wanaCCM wenye kupinga ufisadi wanaweza kuingia kushiriki
katika harakati za ukombozi wa Taifa.
Hata
hivyo aliwataka wanachama wa Chadema kuacha tofauti ya vyama bali wote
waunganishe nguvu zao kuwashawishi wanaCCM ambao wanachukizwa na matendo
ya viongozi wao washiriki katika mapambano kulirejesha taifa kuwa na
viongozi wanaofuata msingi ya kimaadili.
“
Taifa hili lina mpasuko kutokana na vyama vingi ambavyo vinawagawa
wananchi kiitikadi na rangi za bendera na kusahau kujenga umoja
wakutetea maslahi ya wananchi wanyonge” alisema Mbowe na kuongeza kuwa.
Naye
Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu , alisema kuwa
Chadema hakikatai mfumo wa wananchi katika kuchangia shughuli za
maeneleo bali kinachosisitiza ni kwamba fedha zinazopatikana zitumike
kuwalekea maendeleo wananchi wake na si kutajirisha kundi la viongozi
wachache.
Kwa
mujibu wa Naibu Katibu Mkuu huyo wa Chadema Zanzibar,uchangiaji wa
shughuli za maendeleo ulikuwepo hata katika serikali ya awamu ya kwanza
na Mwalimu Julius Kambarege Nyerere, lakini matunda ya uchangiaji huo
yalionekana kwa uboreshaji wa huduma za kijamii, elimu, afya na maji.
Hivyo alisema , ni wajibu wa Serikali inapokusanya kodi , ziwanufaishe wananchi katika kuboresha maendeleo yao badala yakuachiwa wananchi kugharamia uchangiaji wa kila jambo.
SOURCE: John Nditi, HABARILEO Morogoro
Post a Comment