Mchakato
wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kumpata mgombea wa
nafasi ya uenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyamakombo wilayani Bunda,
umeingia dosari, baada ya kundi la mgombea mmoja kushambulia kundi la
mgombea mwingine kwa mawe na mishale.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Mariwanda, Paul Hongo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa 7 usiku katika kijiji hicho.
Hongo alisema tukio hilo limesharipotiwa katika kituo kidogo cha polisi cha Mugeta na inadaiwa kuwa kundi hilo lililokuwa na mawe na pinde lilivamia watu hao na kuanza kushambulia kundi lingine.
Watu walionusurika katika tukio hilo, Webiro Kiharata na Mstapha Mohamed, wamefungua kesi ya kutishiwa kuuawa kwa silaha.
“Mimi nilisikia wananchi wakipiga yowe nilipofika tu katika eneo la tukio nikiwa na pikipiki yangu watu, hao wakaongea kiluga kwamba wanishambulie ndipo wakaanza kurusha mishale upande wangu pamoja na mawe," alisema.
Polisi walisema kuwa wanaendelea na upelelezi kuhusu tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa waliohusika ili waweze kufikishwa mahakamani.
Mwenyekiti wa CCM tawi hilo, Elly Mazimoto, alisema kuwa tukio hilo lilihusishwa na makundi yote mawili kutuhumiana kwamba kuna mazingira ya rushwa. Alisema kuwa tukio hilo lilitokea siku moja tu kabla ya kura za maoni kufanyika kwa mara ya pili, baada ya ule wa awali uliofanyika Oktoba 31, kufutwa.
Kufuatia ushindi huo Mesinya alikata rufaa kwenye kamati ya siasa ya kata hiyo, akidai kwamba katika uchaguzi huo kulikuwa na mizengwe kadhaa, ambapo kamati ya siasa ya kata iliamuru uchaguzi huo urudiwe tena ili haki iweze kutendeka.
Hata hivyo, pamoja na viongozi wa CCM wilaya, akiwemo mjumbe wa NEC, Boniphace Mwita, mwenyekiti wa wilaya Chacha Gimanwa na Katibu msaidizi wa wilaya hiyo Sosthenes Mitti, kusimamia zoezi hilo, uchaguzi huo haukuweza kurudiwa kutokana na kuwepo wanachama wengine hewa kutoka vijiji jirani kutaka kupiga kura.

CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق