Kikosi cha timu ya Zanzibar Veterani kilichotoana jasho na timu ya
Nigeria Veterani katika uwanja wa Amaan Zanzibar katika mchezo wao wa
kirafiki wa kimataifa kukuza mchezo huo Visiwani na kutowa hamasa kwa
Wachezaji Vijana kuinua viwango vyao vya mchezo na Zanzibar kwa jumla.
Kikosi cha timu ya Nigeria Veterani waliotoa sare na timu ya Zanzibar
Veterani wakionesha mchezo mzuri na wakitaalam kuonesha wakati wao jinsi
mpira uliovyokuwa ukichezwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali
Suleiman, akisalimiana na wachezaji wa Zanzibar Veterani akimpa mkono
mchezaji Amour Azizi (Kijeba) kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa kimataifa
uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali
Suleiman, akisalimiana na wachezaji wa Zanzibar Veterani akimpa mkono
mchezaji Haji Mwinyi kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa kimataifa
uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wachezaji wa timu ya Zanzibar Veterani wakisalimiana na wachezaji wa
Nigeria Veterani kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki wa Kimataifa
uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mchezaji mkongwe wa Timu ya Taifa ya Zanzibar na Tanzania Shabani
Ramadhani akisalimiana na Mshauri Ufundi wa Nigeria Veterani Engr.
Iyenemi N Ameiye, kabla ya kuaza kwa mchezo huo uliofanyika uwanja wa
amaan.
Mchezaji wa Veterani Zanzibar Haji Mwinyi akifudga balo la kwanza kwa
timu yake dhidi ya timu ya Nigeria Veterani. katika mchezo wa kirafiki
wa kimataifa uliofanyika uwanja wa amaan.
Post a Comment