MFANYE MKEO AU MPENZI WAKO AWE NA FURAHA MUDA WOTE KWA KUFANYA YAFUATAYO


1. Mpigie simu hata mara moja kwa siku, hata ikitokea umebanwa sana na kazi tuma hata ujumbe mfupi tu
2. Msikilize kwa makini aongeapo
3. Msifie/Mpongeze kwa dhati mara kadhaa uwezavyo
4. Chunguza kwa makini vitu anavyovipenda na asivyovipenda
5. Jenga tabia ya kumnunulia zawadi sio lazima mpaka ukiwa unatoka safari
6. Jitahidi kuwa mnatoka wote sio lazima mpaka uwe na marafiki zako,mfano chakula cha jioni nk
7. Kuwa na upendo kwake, usiwe mtu wa fujo ugomvi hasira
8. Onyesha unamjali kwa kutanguliza mahitaji yake kabla ya kwako
9. Fanya mambo upendayo mfano mwanaume unaweza ukawa unapenda kuangalia soka, kunywa kidogo na mwenzi wako anapenda movie, swimming sasa hapo ukifanya yako hakikisha unamsupport upande wake ili furaha yenu ikiutane
10. Kuwa muwazi kwa baadhi ya vitu ambavyo unahisi anahitaji maelezo yaliyojitosheleza
By:-  Mike Tee Senior

Post a Comment

أحدث أقدم