Alisema anavyoamini yeye wakifanikiwa kufanya
jambo hilo litawapa heshima, pia itawashtua wawekezaji wengine wenye
lengo la kuhujumu nchi kwa kisingizio cha uwekezaji.
“Yaani mimi sitaki kumnyooshea mkono kiongozi
yeyote lakini najiuliza jambo hili limewezekanaje, tuna kila sababu ya
kutaifisha kwanza ameleta ‘document fake’ (nyaraka) feki, hivyo
tuichukue ile mitambo tuikabidhi Tanesco, Serikali ituunge mkono,”
alisema Serukamba.
Alisema pia fedha hizo zinaweza kurejeshwa iwapo
Benki Kuu (BOT) watawaandikia Benki ya Stanbic kulipa fedha hizo kwa
sababu hazikufuata taratibu za kibenki zinazotakiwa hasa kuruhusu fedha
kiasi kikubwa zaidi ya milioni 10 kuchukuliwa taslimu.
Mbunge Ester Bulaya (Viti Maalumu CCM) aliliambia
Bunge kuwa yupo tayari kuwachukua vijana waliokosa mikopo, wanawake
wanaokosa huduma bora ya afya kuandamana, iwapo hatua za kisheria
hazitachukuliwa dhidi ya waliohusika ufisadi kwenye akaunti ya Escrow.
Alisema kuwa wahusika wote wanapaswa kuchukuliwa
hatua kwa kusababisha aibu kubwa kwa nchi na mateso kwa wananchi, ambapo
aliitaka Serikali kuwa makini na wawekezaji ili kuepuka kupokea
matapeli.
“Hawa viongozi waliopewa hizo fedha ambazo wanadai
kwamba ni michango, wanashangaza, hii ni aibu kwa sababu mwingine
aliyedai kuwa ni mchango taarifa zinaonyesha kwamba ziliingia kwenye
akaunti ya shule hizo kwa saa 48 kisha zikatolewa zote bila hata bodi
kuridhia,” alisema Bulaya.
Bulaya alisisitiza kuwa mazingira yanaonyesha kwamba viongozi waliopewa fedha hizo ilikuwa ni kama zawadi kwa kukamilisha dili.
Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP) John Cheyo,
alieleza kukerwa na viongozi wa Serikali wanaosimama kusisitiza kuwa
fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow hazikuwa za Serikali.
“Siyo lazima uwe na digrii kuelewa hili, viongozi
hao wanaposimama hapa na kukana kuwa fedha hizo hazikuwa za Serikali
wananchi wanakasirika, nataka hata kulia ‘it’s not possible’ Serikali
maskini inayotegemea wafadhili kukataa fedha namna hiyo,” alisema Cheyo.
Alisema mbaya zaidi ni kwamba fedha hizo zilizopaswa kulipwa kwa IPTL zimelipwa kwa mtu wa tatu.
“Mungu wangu, Mungu wangu, huyo mtu kwa ujanja
ujanga alipokea hiyo fedha, kisha akafunga akaunti husika ‘we can’t see
the money has gone’, hatua zichukuliwe kwa wote waliohusika IPTL ni
kidonda ndugu kwa miaka 20,” alisema Cheyo.
- Mwananchi
- Mwananchi
Post a Comment