SOKO
la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS&
CRAFTS MARKET limetea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa
zote za wafanyabiashara zililopo katika soko hilo
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika
kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za
kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.
Mulongo
ambaye alifuatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona
maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima
moto na kusababisha hasara kwa wananchi.
“Sitakubali
kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa
uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama
Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya” amesema Mulongo
Chanzo
cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku
yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto
kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao. (Habari picha
kwa hisani ya Woindeshizza Blog)









إرسال تعليق