![]() |
Imeandika na Josephine B Mramba
Dondoo Kutoka Kikao cha Ndani ya Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana Dodoma kilichofanyika Ofisi za TAMISEMI.
Kikao rasmi cha kujadili sakata la IPTL/ESCROW namna wahusika watakavyowajibishwa au kuokolewa.
1.Misimamo ya Mawaziri tofauti tofauti.
Mwigulu
Nchemba ambaye ni Naibu waziri wa Fedha anatajwa kuwa Waziri wa kwanza
kuonesha msimamo wake wazi wazi kuwa Sakata la IPTL/ESCROW ni hujuma
dhidi ya Uchumi wa Nchi.acharuka,AAGIZA MALI ZOTE NA PESA ZOTE
ZILIZOLIWA, ZILIZOTAWANYWA ZIKAMATWE.Naibu huyu ambaye mara kadhaa
amekuwa akitajwa na vyombo vya habari kwa juhudi zake za kuokoa matumizi
mabaya ya fedha na hata Watanzania wengine kuamua kumbatiza jina la
Sokoine wa pili ikiwa ni kufuata nyayo za aliyewahi kuwa Kiongozi Makini
Nchini hayati Moringe Sokoine.
Mwigulu ndani ya kikao hicho cha siri
anatajwa kuendeleza ujasiri wake kuhusu mambo yenye masilahi ya Taifa.
Wakati watu na tetesi mbalimbali zilikuwa zinaongelea kujiuzulu, Mwigulu
amejitokeza kwenyw kikao hicho na kusema CAG ameshamaliza utata, sasa
mali zote, fedha zote za IPTL zikamatwe na wahusika wote wakamatwe.
Nanukuu kama nilivyosikia"Tumezoea
kusema eti tumewajibisha watu kwa wao kujiuzuru, "Kujiuzuru ni kupewa
Likizo ya kwenda kula fedha ulizo ziiba"anasema Mwigulu, Hili ni jambo
la mazoea, sasa, CAG ameshasema pesa zile zilikuwa mali ya umma, sasa
zikamatwe zote, na wahusika wote wakamatwe"
Mwigulu
alienda mbali zaidi na kusema hata ambao walishastaafu na wamehusika
kulihujumu taifa wakamatwe na akaunt zao zikamatwe, zifilisiwe
zirudishwe kwa wananchi.
Katika
hatua nyingine Naibu huyo anayeshughulikia mambo ya sera, Mwigulu
ameagiza mtumishi wa TRA aliyepewa 1.6bilion afukuzwe kazi, akamatwe, na
akaunti ifilisiwe fedha irudi serikalini. Pia mitambo ya IPTL ikamatwe
irudishwe serikalini. Utamaduni wa watu kujiuzulu na kuhesebu kuwa ni
adhabu ni jambo la zamani, sasa ili kukomesha wizi, uzembe na ufisadi
sasa tuwakamate wahusika wote, tuwafilisi na tuwaweke ndani na
tuwafunge.
Habari
za uhakika kutoka kikao cha baraza la Mawaziri zinasema, jana Mwigulu
Nchemba aliongea kwa sauti ya mamlaka mbele ya Waziri mkuu nakusema
kujiuzuru sio adhabu stahiki kwa wizi Mkubwa kama huu wa Mali ya
Umma,Hisia hizo zikiwa zimegubikwa na maisha yake halisi ya umasikini
aliyokulia na huku akihusisha Wizi wa fedha na hujuma dhidi ya
Watanzania Masikini.Mbunge huyo wa iramba anasisitiza kwa kusema "
Tazama wanafunzi, watoto wa masikini zaidi ya elfu 40 wamekosa mikopo,
madawa hospitalini hakuna masikini wanakufa, watu wasio na hatia
wanafungwa kwa kukosa michango ya maabara, walimu wanadai, wazabuni
wanauziwa nyumba zao na mabenki huku wakiidai serikali kwa huduma
walizotoa, leo wezi tuwape adhabu ya kujiuzuru? Tuwape likizo ya kwenda
kutumia fedha walizo waibia masikini? Hapana, "Enough is enough" ndg
Waziri mkuu tuwakamate, tuwafilisi, tuwafunge. Pesa na mali virudi
serikalini."
Kwa yule mtumishi wa TRA aliyekula
fedha za IPTL zaidi ya 1.6 B,Mwigulu akatoa agizo kuwa "Nimemwagiza
kamishna wa kodi amfukuze kazi yule wa TRA iliyoko chini ya wizara
yangu, na afilisiwe, pia mitambo na kodi vikamatwe, na wahusika
wakamatwe. Hatuwezi kuendeleza mazoea ya kufunga masikini na kuwapa
likizo wezi wakatumie fedha. Walio serikalini na walioko kwenye siasa
wakamatwe na tuwafilisi fedha irudi serikalini."
Taarifa za uchunguzi zunasema tayari TRA imechukua hatua."
Naibu Waziri KILIMO Mh.Godfrey Zambi wanusurika Kukunjana na Werema(Mwanasheria Mkuu wa Serikali).
Wakati kikao kikiwa kimepanda joto la
juu,Mawaziri wakifikia makubaliano kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na madini Maswi na Mawaziri waliohusika ni lazima waachie ngazi,Ndipo
Werema alipotaka kumkunja Mh.Zambi baada ya kutoleana maneno machafu
dhidi ya mali ya uma.
Madai yanakwenda mbali kuwa,Zambi
alikuwa anapigia kelele kuwa inawezekanaje Mwanasheria mkuu kubariki
wizi wa Fedha za Umma?.Ni wapi watu wa msoma wakasifika kwa wizi wa mali
za Umma?.Chokochoko hizo ndio zilipelekea Ugomvi kati ya Zambi na
Werema.
Mbali
na Mawaziri hao,Mh.Tibaijuka amekuwa Mwizi wakwanza wa IPTL kukubali
kuwajibika katika sakata hili mbele ya kikao cha baraza la Mawaziri.
Ni wakati Muafaka
sasa kwa Watanzania wote kuunga kupaza sauti kama akina Zitto
walivyofanya,Kuunga mkono zaidi Machozi ya akina Mwigulu waliojitolea
kutetea Masikini wakati huo huo wanahujumiwa na Mawaziri wenzao ndani ya
Chama tawala,Mwigulu ameanua kujilipua Mzima mzima bila kujali yeye ni
nani ndani ya Chama kwa Malengo kuwa CCM haipo tayari kukumbati waovu na
wezi.
|
![]() |
Imeandika na Josephine B Mramba
Dondoo Kutoka Kikao cha Ndani ya Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana Dodoma kilichofanyika Ofisi za TAMISEMI.
|
إرسال تعليق