Denis Mtima na Gabriel Ng’osha LILE
sakata la mtoto wa miezi 6 (pichani) kufia mahabusu ya Kituo cha Polisi
cha Kova, Mbezi Kwamsuguri, Dar linaendelea! Safari hii, mama wa mtoto
huyo, Meradi Meshack ameibua mazito akiwataja polisi jamii kuwa ndiyo
chanzo cha kifo cha mwanaye.
Mtoto Thomas wa miezi 6 aliyefia mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Kova, Mbezi Kwamsuguri, Dar enzi za uhai wake.
Awali ilibainika kuwa, mtoto huyo
aliyefariki dunia Novemba 18, mwaka huu wakati mama yake akiwa amewekwa
kituoni hapo kama mhalifu, polisi wa kituo hicho walitajwa kuhusika.
Akizungumza na waandishi wetu, mama huyo alisema yeye na mtuhumiwa wake aliyemtaja kwa jina la mama Na walikuwa wakidaiana fedha za upatu ambazo alikuwa akimdanganya kuwa wanachama wenzake bado hawajatoa.
Akizungumza na waandishi wetu, mama huyo alisema yeye na mtuhumiwa wake aliyemtaja kwa jina la mama Na walikuwa wakidaiana fedha za upatu ambazo alikuwa akimdanganya kuwa wanachama wenzake bado hawajatoa.
Mama wa mtoto huyo akilia kwa uchungu msibani.
Baada ya usumbufu wa muda mrefu ndipo
wakapishana maneno, mwanamke huyo akampeleka polisi akidai alitaka
kumpiga. “Nilifuatwa na polisi jamii wawili na si polisi wenyewe. Mimi
nilikuwa na mume wangu, niliwaambia mwanangu anaumwa nitakwenda kesho
lakini hawakukubali, wakanitukana na kunichukua kwa mabavu huku mwanangu
akiwa na hali mbaya na walimuona.
Ndugu na majirani waliofika kumfariji mfiwa(mama wa mtoto), Meradi Meshaki, (kulia).
“Shangazi yangu na mume wangu walinifuata
wakitaka kuniwekea dhamana, wale polisi jamii wakakataa, wakanitupa
mahabusu. Mwanangu akazidi kuwa na hali mbaya zaidi maana hali ya hewa
mle mahabusu ilikuwa ni nzito sana.Baba wa marehemu Thomas, aliyefahamika kwa jina moja la Paschal (aliyekunja mikono).
“Usiku nilipitiwa na usingizi,
niliposhituka usiku wa manane nikamuona akikohoa na kupumua kwa shida,
baadaye akalegea na kuwa kama amelala, nikawaita wale polisi jamii
lakini hawakuja. “Ndipo alfajiri, mmoja wao akaja, akanitazama kisha
akaondoka zake. Akaja mwingine, akamshika mwanangu akawa kama
ameshtuka, akaniambia niondoke haraka nimpeleke hospitali.Waombolezaji wakiwa msibani hapo.
“Kumbe wakati anasema hivyo alishajua mwanangu amefariki dunia,
inauma sana kwa kweli! Nilitoka na kilio kwani nilishampoteza mtoto
wangu na wao sikuwaona tena! Walikimbia! Huu ni ukatili wa hali ya juu,”
alisema mwanamke huyo.Naye mjumbe wa eneo hilo, Rashid Sultan alisema taarifa za kifo cha mtoto huyo alizipata na kuwatupia lawama polisi jamii waliojichukulia uamuzi wa kumweka mahabusu mwanamke huyo tena akiwa na mtoto mchanga wakati kituo hicho ni kidogo na hakilazi wahalifu nyakati za usiku na hutakiwa kufungwa saa 12 jioni.
Inadaiwa kuwa, chanzo cha mtoto huyo kufariki dunia ni kukosa hewa huku akiwa anasumbuliwa na kifua. Hadi Uwazi linakwenda mitamboni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura hakuwa akipatikana kwenye simu yake ya mkononi ili kuelekeza anachokijua.
Marehemu alizikwa Novemba 19, mwaka huu kwenye Makaburi ya Mbezi Kwamsuguri jijini Dar. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.
إرسال تعليق