| Mwanamke akifurahia uamuzi wa mahakama dhidi ya rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak REUTERS/Asmaa Waguih |
Na Sabina Chrispine Nabigambo
Mahakama kuu nchini Misri jana Jumamosi imemwondolea mashitaka ya mauaji
rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak kutokana na vifo vya
waandamanaji wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya mwaka 2011 baada ya
kujaribu kutaka kusalia tena madarakani huku akiwa ameongoza nchi hiyo
kwa miaka 30.
Uamuzi huo umechochea hasira ya wapinzani wa Mubarak ambapo karibu watu
1000 walikutana katikati mwa jiji la Cairo kupinga serikali.
Wizara ya afya imesema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kufariki dunia
wakati Polisi wa kutuliza ghasia nchini Misri wakijaribu kuwatawanya
waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga uamuzi ya mahakama nchini
humo.
Aidha mahakama imemwondolea rais huyo wa zamani mashataka ya rushwa,
lakini ataendelea kubaki kizuizini kwa sababu anatumikia kifungo cha
miaka mitatu katika kesi nyingine ya rushwa.
Maaafisa wengine saba waliohudumu kwenye serikali ya Mubarak akiwemo
waziri wa zamani wa mambo ya ndani anayeogopwa Habib al Adly pia
wamefutiwa mashitaka ya mauaji ya watu 800 waliouawa katika mapinduzi
hayo.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
إرسال تعليق