![](http://www.whothehelldoeshethinkheis.com/wp-content/uploads/2014/03/Homer-Simpsons-Music-Headphones-Anime.jpg)
Kinachofurahisha zaidi ni kwamba, ladha ya muziki
wa wakongwe hao ya awali, bado ipo kwa kiwango kile kile. Hakuna ubishi
kwamba kila unaposikiliza tungo za mashairi yao, unapata ujumbe ule ule
uliokusudiwa sanjari na burudani yake.
Takribani miongo miwili sasa kumekuwapo na mfumko
wa wanamuziki wanaojiita wa kizazi kipya. Wanamuziki hawa wamekuwa
wakipiga muziki katika mahadhi yanayojulikana kama Bongo Fleva.
Muziki wa zamani uliopigwa na wakongwe niliowataja
hapo juu na wengine kama hao una tofauti kubwa na ule wa Bongo Fleva.
Tofauti hiyo ipo kimaudhui, kimuundo, hata uwasilishwaji wake.
Lakini kubwa zaidi ni kwamba muziki wa Bongo Fleva umeondoa kwa kiwango kikubwa utambulisho wa awali wa muziki wa kitanzania.
Kwa kiasi kikubwa jambo hilo limechangia kupoteza umaarufu wa muziki wa kitanzania kwenye medani za kimataifa.
Je, nini chimbuko la tatizo?
Kuna changamoto nyingi zinazoukabili muziki wa
kitanzania. Kwa kiasi kikubwa, changamoto hizo zimechangia kupotea kwa
muziki wa asili. Siyo hivyo tu, bali pia zimechangia kudunisha muziki
nchini.
Charles Mohamed Kayoka ni mwalimu wa sanaa katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), anazitaja baadhi ya changamoto hizo
kuwa ni pamoja na utandawazi.
Anasema kuwa ujio wa teknolojia, umerahisisha mambo mengi kasa katika masuala ya muziki.
Anafafanua kwamba hali hiyo imesababisha vyombo
vilivyohitaji kupigwa na kundi la wanamuziki, sasa kufanywa na mtu mmoja
kwa kutumia kinanda kimoja tu.
“Msaada wa kompyuta, unatosha kabisa kumwezesha
msanii kutengeneza wimbo anaoutaka kwa saut ya ala anayoitaka, hatimaye
akaingiza muziki huo sokoni. Jambo hili limechangia uvivu na kutojituma
kwa wanamuziki wetu,” anasema - (Mwananchi)
Post a Comment