Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai
Zanzibar (DDCI), Salum Msangi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa
tukio hilo lilitokea juzi saa tano asubuhi katika hoteli hiyo.
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni waandishi wa
habari, Munir Zakaria wa Channel Ten na Kuruthum Ali wa TBC ambao
walikuwa kazini. Wengine ni Ramadhani Mohammed (25), Wadi Ame Khamis
(35), Ashraf Suleiman (36) na Nadir Ali Juma (28).
Alisema mwekezaji huyo anashikiliwa pia kwa
kumiliki silaha inayodaiwa kutumika katika shambulio hilo aina ya Gamo
yenye namba 04-4L-720/70-07 ambayo imetengenezwa Hispania.
Alisema kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (3) cha Sheria
ya Silaha namba 2 ya mwaka 1991 na Kifungu namba 19 cha Sheria ya
Silaha Tanzania Sura ya 223, mtu yeyote akiwa Tanzania na Zanzibar
haruhusiwi kutumia au kumiliki silaha pamoja na risasi. Alisema taratibu
za kumfikisha mahakamani zimeanza.
Katika tukio jingine, Msangi alisema polisi pia
inamshikilia raia wa Poland, Artur Miarka (52) kwa tuhuma za kukutwa na
bunduki aina ya BSA air Rifle na risasi zake pamoja na darubini ya
kumsadia kuona mbali.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo la
Pwani Mchangani, Mkoa wa Kaskazini Unguja na baada ya kuhojiwa alisema
amekuwa akitumia silaha hiyo kwa muda wa miaka mitatu Visiwani hapa.
Alisema kutokana na matukio hayo, polisi imetoa
wiki moja kwa wawekezaji wote wanaomiliki silaha Zanzibar kuzisalimisha
katika vituo vya polisi kabla ya kuanza kwa msako katika hoteli zote
Unguja na Pemba.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق