Polisi
hapa mjini Ifakara wamepata wakati mgumu kumwokoa bwana mmoja
aliyefahamika kwa jina la Nurdin Mangula, baada RAIA wenye hasira Kali
kutaka kumuua wakimtuhumu kuiba watoto na kuwaua kisha kuchukua baadhi
ya viungo na kuviuza kwa baadhi ya wafanyabiashara.
Jamaa
huyo ambaye mke wake ni hakimu wa mahakama ya mwanzo aliokolewa na
polisi waliotumia nguvu kubwa kumnusuru asiuawe na RAIA wenye hasira
Kali.
Wiki
mbili zilizopita kuna watoto wawili walipotea katika mazingira ya
kutatanisha na mmoja kupatikana akiwa tayari ameshakufa na baadhi ya
viungo akielwa hana.
Mtuhumiwa
huyo ambaye ana undugu na makamu mwenyekiti wa CCM Philip Mangula
amekutwa na watoto watatu kwenye gari aina ya Noah na mmoja akiwa tayari
amekufa.
Pamoj na kuokolewa na polisi watu wamefanikiwa kuichoma moto nyumba yake na magari mawili. kuchukua kila kitu ndani ya nyumba.
Chazo: ZeroSeventytwo
إرسال تعليق