MAMBO
ya urithi! MOJA ya nyumba mbili zilizoachwa na marehemu Muhidin Maalim
‘Gurumo’, iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, ambayo ndiyo anayoishi
mkewe Pili Saidi, ipo sokoni baada ya watoto wake kung’ang’ania iuzwe.
Moja ya nyumba mbili zilizoachwa na marehemu Muhidin Maalim ‘Gurumo’.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, watoto hao wapatao sita,
wamemlazimisha mama yao huyo wa kambo kukubaliana nao kuhusu jambo hilo,
wakiahidi kumpatia fungu lake, kwani wao wanataka kugawana mali
iliyochumwa na baba yao.
“Yule mama yupo kwenye kipindi kigumu kweli, maana wale watoto hawana
ushirikiano naye kabisa, sijui ataishi kwenye mazingira gani na sidhani
kama wanampa msaada wowote wa kujikimu kimaisha,”kilisema chanzo chetu.
Bi. Pili alipoulizwa juu ya ukweli wa
habari hizo, alikiri nyumba kuwa njiani kuuzwa kwani yeye hana uwezo wa
kupingana na watoto wa marehemu, hivyo amekubaliana nao ili kujiepusha
na mabalaa mengine.
Marehemu Muhidin Maalim ‘Gurumo’ akiwa na mkewe Pili Saidi enzi za uhai wake.
Marehemu Muhidin Maalim ‘Gurumo’ akiwa na mkewe Pili Saidi enzi za uhai wake.
“Ni kweli hii nyumba watoto wa marehemu wote wamekubaliana kuiuza ili
wagawane na wameahidi kunipa fungu langu, siwezi kupingana na hilo kwa
kuwa mimi sikubahatika kumzalia, japo sijui hatma ya maisha yangu
nitakapoondoka humu ndani maana hawa vijana hatuna ushirikiano mzuri kwa
sasa.”
Alisema hata gari ya marehemu aliyozawadiwa na Diamond ilitaka
kuuzwa, lakini akasimama kidete kuitetea kwa kuwa msanii huyo alimwambia
kwa kuwa mumewe amefariki basi itakuwa mali yake na kusema inamsaidia
kujikimu kimaisha kwani anaifanyia biashara.
Post a Comment