Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar
es Salaam kuhusu ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5 litakaloanzia
eneo la Aghakani na kuishia Coco beach, ujenzi huo unaotarajiwa kuanza mapema
mwakani na unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Korea Kusini ,lengo
ni kupunguza msongamano wa magari katika daraja la Serender.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kulia),akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam kuhusu ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5
litakaloanzia eneo la Aghakani na kuishia Coco beach, ujenzi huo unaotarajiwa
kuanza mapema mwakani na unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Korea
Kusini ,lengo ni kupunguza msongamano wa magari katika daraja la
Serender,kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. Juma Iyombe.Picha
na Lorietha Laurence –Maelezo
---
| Na Beatrice Lyimo |
Zaidi
ya Bilioni 110 zinatarajia kutumika katika ujenzi wa daraja lenye urefu wa
kilometa 7.5 ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli alisema daraja hilo litaanzia eneo la Aghakani na kuishia Coco
beach.
Waziri
Dkt. Magufuli alisema daraja hilo litakalojengwa kwa msaada wa Serikali
ya Korea Kusini litakuwa na njia nne na barabara mbili za huduma kwa kila
upande lenye uwezo wa kupitisha magari elfu 61 kwa siku .
“Serikali
ya Korea Kusini imemaliza mradi wa ujenzi wa daraja la Kikwete pamoja na
barabara ya Malagalasi Mkoani Kigoma na sasa tumewaomba waendelee kutoa
msaada kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani Dar es Salaama ili kupunguza
msongamano wa magari”, alisema Dkt. Magufuli.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu kutoka TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale
amebainisha kuwa wataalamu kutoka Korea Kusini wameshafanya Upembuzi
yakinifu uliomalizika hivi karibuni, hivyo ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa
kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao.
Aliongeza
kuwa daraja hilo litakalofahamika kwa jina la New Salender Bridge
litaunganishwa na barabara ya Ally Hassan Mwinyi kutokea Aghakani na kwa upande
mwingine litaunganishwa na barabara ya Chole iliyopo Masaki.
Serikali
imeweka mikakati mingi ya kupunguza msongamano wa foleni za magari kwa
kuanzisha ujenzi mbadala wa barabara za juu unaotarajiwa kujengwa maeneo ya
TAZARA,Mbagala rangi tatu hadi gerezani, kuanzishwa kwa kivuko cha Dar es
Salaam hadi Bagamoyo.
Pia
utafanyika utanuzi wa barabara nyingine za Dar es salaam kwenda Morogoro
kupitia Chalinze na ile ya Morocco hadi Mwenge na Bagamoyo hadi
Msata.
إرسال تعليق