
Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara, Pius Mboko na
wahifadhi wa wanyamapori,wakimfanyia uchunguzi simba mmoja kati ya saba
waliouawa juzi kwa kuwekewa sumu katika nyama baada ya kudaiwa kula
ng’ombe wa mwanakijiji anayeishi kando ya Hifadhi ya Jamii ya Ikona.
Picha na Anthony Mayunga
----
Na Anthony Mayunga, Mwananchi
Simba saba wamekutwa wamekufa Hifadhi ya Jamii ya Ikona (WMA)
wilayani Serengeti, mkoani Mara baada ya mfugaji mmoja wa Kijiji cha
Park Nyigoti kudaiwa kuwatega kwa sumu, kufuatia ng’ombe wake mmoja
kukamatwa malishoni ndani ya hifadhi hiyo.
Tukio hilo lilibainika juzi ndani ya hifadhi hiyo
Kijiji cha Park Nyigoti, baada ya mfugaji huyo Manyeresa Nguhecha
akiongozana na askari wa Pori la Akiba la Ikorongo na walinzi wa Kampuni
ya Grumeti Reserves na kukuta mizoga hiyo wakati akifuatilia eneo
ambako ng’ombe alikamatiwa.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Elias Chama akiwa eneo
la tukio alisema juzi jioni simba walimuua ng’ombe wa mfugaji huyo,
lakini walifanikiwa kuwafukuza kabla hawajaanza kula nyama.
Chama alidai kuwa gharama ya simba kwa uwindaji wa kitalii ni Sh25 milioni, hivyo wangewindwa wangeingiza Sh175 milioni.
Mtuhumiwa anadaiwa kutoroka kwa kutumia pikipiki
na kwamba, alikuwa miongoni mwa wanachama wa jumuiya hiyo waliojitokeza
kugombea nafasi ya mwenyekiti na baadaye alijitoa. Madaktari wa Mifugo
Wilaya ya Serengeti, Tito Kagize na Ahmed Lugelo walisema sumu hiyo
ilisababisha damu kuvujia ndani ndiyo.
“Tunahisi ni sumu maana dalili zake zipo, kwanza
vifo vya wanyama wengi kwa muda mfupi, chanzo cha vifo ni kimoja
wamekula nyama ya ng’ombe na inaonekana walikula zaidi kitoto cha ndama,
matokeo zaidi tunasubiri majibu ya mkemia maana vipimo vyote
vinapelekwa huko,” alisema Dk Kagize.
Hata hivyo, msako ulioendeshwa na polisi nyumbani
kwa mtuhumiwa unadaiwa kukuta ngozi ya ng’ombe iliyoraruliwa, nyama
iliyokuwa imebaki na chupa moja iliyokuwa na harufu ya sumu ambayo
haijajulikana.
إرسال تعليق