JINSI RUGIMARILA ALIVYOWAPONZA MAASKOFU NA HATIMAYE KANISA KATOLIKI KUINGIA KATIKA KASHFA ITAKAYOWAFILISI UNAJUA ILIKUWAJE....
Pichani ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Nchini Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo Picha na Maktaba
Na Karoli Vinsent,Dodoma
KANISA katoliki nchini limeingia kwenye Kashfa nzito ambayo halitoliacha salama kanisa hilo kubwa nchini na Duniani,baada ya maaskofu wake wajuu kupokea pesa za kutoka kwa bwana James Rigimalira ni Mmiliki wa kamnpuni VIP ambaye anatajwa kuliibia taifa kupitia Mkataba wa kinyonyaji IPTL
Hayo yamegundulika mda huu Bungeni Dodoma wakati ikisomwa ripoti ya mkaguzi mkuu wa Serikali CAG ilikuwa inalikagua ufisadi huo na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu ya Serikali PAC Zitto Kabwe ambapo Zitto alisema Mkurugenzi wa VP engineering bwana James Rugimarila aliwaangizia pesa, Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Bukoba, Dk. Methodius Kilaini ambaye ameingiziwa milioni 80 kutoka kwa bwana James Rugimalira pasipo sababu yeyote huku ikizingatia huyu ni kiongozi wa dini.
Mbali na Askofu Kilaini,Zitto Kabwe alimtaja Askofu Mwingine wa kanisa Katoliki kutoka Jimbo kuu la Dar es Salaam Askofu Mzigilwa naye amepewa Milioni 40.4 pasipo sababu ya msingi.
إرسال تعليق