RAIS Jakaya
Kikwete amewasili nchini leo akitokea
Marekani ambako alienda kutibiwa tezi dume na kutoa wito kwa wanaume
kuhakikisha wanapima tatizo hilo na wananchi kw aujumla kuwa na mazoea ya
kupima afya zao.Pamoja na
kuelezea historia ya ugonjwa wake ambapo anasema ilimchukua miezi nane
kumwambia mkewe na baraza la mawaziri
kumng’ang’ania asiwaambie wananchi wakati anakwenda kufanyiwa operesheni, amesema
ni kitu chema kwa wanancghi kujenga mazoea ya kupima afya zao.
Anasema
kutokana na mazoea ya kupima afya kila mwaka, madaktari waliweza kuabini tatizo
la pingili katika shingo yake mika kadhaa iliyoppita na pia kubaini tatizo la
chembe za kansa kwenye tezi dume.
Akiwa uwanja
wa ndege baada ya kuwasili Rais alikuwa na mazungumzo na taifa kupitia vyombo
vya habari na TBC ikirusha moja kwa moja.Rais alisema
kwamba alibainika kuwa na chembe za kansa katika tezi dume na kwamba amefanyiwa operesheni na hali yake sasa
ni bora.
Alisema
kwamba suala la Dodoma (escrow) halijui vyema akilijua atawaambia wananchi.

Post a Comment