Rais awasili na kueleza umuhimu wa kupima afya, alionwa na chembe za saratani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Prof. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Marekani kwenye Matibabu.

RAIS Jakaya Kikwete  amewasili nchini leo akitokea Marekani ambako alienda kutibiwa tezi dume na kutoa wito kwa wanaume kuhakikisha wanapima tatizo hilo na wananchi kw aujumla kuwa na mazoea ya kupima afya zao.Pamoja na kuelezea historia ya ugonjwa wake ambapo anasema ilimchukua miezi nane kumwambia mkewe na  baraza la mawaziri kumng’ang’ania asiwaambie wananchi wakati anakwenda kufanyiwa operesheni, amesema ni kitu chema kwa wanancghi kujenga mazoea ya kupima afya zao.
Anasema kutokana na mazoea ya kupima afya kila mwaka, madaktari waliweza kuabini tatizo la pingili katika shingo yake mika kadhaa iliyoppita na pia kubaini tatizo la chembe za kansa kwenye tezi dume.
Akiwa uwanja wa ndege baada ya kuwasili Rais alikuwa na mazungumzo na taifa kupitia vyombo vya habari na TBC ikirusha moja kwa moja.Rais alisema kwamba alibainika kuwa na chembe za kansa katika tezi dume na  kwamba amefanyiwa operesheni na hali yake sasa ni bora.
Alisema kwamba suala la Dodoma (escrow) halijui vyema akilijua atawaambia wananchi.

Post a Comment

أحدث أقدم