Ray Rice
Mchezaji wa zamani wa timu ya football ya Baltimore Ravens Ray Rice
ameshinda rufaa yake aliyokua amefungiwa na chama cha mchezo huo NFL
kucheza mchezo huo wa Football ambao ni maarufu nchini Marekani
Mchezaji Ray Rice sasa anaweza kujiunga na timu yeyote baada ya mahakama kuondoa pingamizi alilokua amewekewa na NFL.
Ray Rice alifungiwa mechi 2 mwezi Septemba mwaka huu baada yakubainika
kumpiga wakati huo akiwa mchumba wake Janay. Na baada ya video kutoka
hadharani kwenye tv na mitandao bodi ya NFL ilibadilisha uamuzi wake na
umfungia msimu mzima mchezaji huyo kwa kosa la kumpiga Janay ambaye sasa
ni mke wake..
إرسال تعليق