Na Imelda Mtema MSANII
anayekuja kwa kasi katika tasnia ya Filamu Bongo, Sarbrina Omary ‘Sabby
Angel’ amefunguka kuwa mwanamuziki, Rummy Nanji ‘Bob Junior’ ambaye
kwa hivi sasa ndiye mpenzi wake amembadilisha mavazi yake aliyokuwa
akivaa awali kabla hawajawa pamoja.
Msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia ya Filamu Bongo, Sarbrina Omary ‘Sabby Angel’ akipozi.
Akizungumza na Amani, Sabby alisema kuwa mpenzi wake huyo mara nyingi
anapenda ajitande nguo na kuwa mtoto wa Kiislamu kama asipokuwa katika
ishu za kurekodi kwani anaamini kuwa binti wa Kiislamu anapaswa kuvaa
kiheshima.
Mtoto ‘Sabby Angel’ akiwa na Nanji ‘Bob Junior’.
“Nimekamatika sana, yale mavazi yangu ya awali nimeambiwa ‘stop,’
tukiwa katika mazingira ya kawaida ni lazima nijitande na nionekana
haswa ni mtoto wa Kiislamu,” alisema Sabby.
Post a Comment