Samsung yapongezwa kwa kukuza teknolojia nchini

Kampuni ya Samsung Electronics Tanzania imepongezwa kwa kusaidia kukuza teknolojia ya mawasiliano na kukomesha bidhaa bandia nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu, alitoa pongeza hizo wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Samsung Galaxy note 4 jijini Dar es Salaam jana.

Alisema jitihada za kampuni hiyo kuendelea kuleta bidhaa zenye ubora, ni ishara nzuri kwamba Tanzania ipo mstari wa mbele wa mabadiliko ya teknolojia yanayojitokeza kote barani Afrika.

Alisema kupitia bidhaa zao mbalimbali, Samsung inachangia ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira za kudumu na za muda kwa vijana.

Alisisitiza kuwa teknolojia ambayo ni uti wa mgongo wa viwanda, kupitia mawasiliano imewaunganisha wafanyabiashara, wawekezaji na raia wa kawaida katika simu za viganjani.

Akizungumzia kuhusu bidhaa feki, alisema zina madhara makubwa katika utendaji mzima wa shughuli za kiuchumi na kutoa wito kwa wadau wote wenye nia njema kama ilivyo kampuni hiyo kukomesha vitendo vibaya vya kusheheni bidhaa feki nchini.


Wakati huo huo, Meneja Mkurugenzi wa Samsung, Mike Seo, wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Samsung Galaxy note 4, alisema kampuni yake imesaidia katika maendeleo ya simu za mkononi na sekta ya habari na mawasiliano.

Seo alisema vifaa vyao vimesambaa nchini kupitia mamlaka za usambazaji zinazohakikisha taifa linafaidika katika kila nyanja ya biashara ya mawasiliano, alisema kabla ya kuingia kwa Samsung nchini, usambazaji wa simu haukuwa wa moja kwa moja bali ilikuwa kupitia wasambazaji ambao hawakunufaisha uchumi wa nchi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Post a Comment

Previous Post Next Post