Meneja
wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (kulia) akiongea na waandishi wa
habari hawapo Pichani, wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya Tutoke na
Serengeti, ambapo Bi.Rukia Athuman Almas toka Kihonda-Morogoro ameibuka
mshindi wa kwanza na kujinyakulia Limo Bajaji mpya yenye thamani ya tsh
milioni tisa, kushoto ni mkaguzi toka bodi ya Michezo ya bahati nasibu.
Meneja
wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (kulia) akiongea kwa njia ya simu
ya mkononi na Rukia Athuman Almas ambaye ni mshindi wa kwanza wa
promotion ya Tutoke na Serengeti, kushoto ni mkaguzi toka bodi ya
Michezo ya bahati nasibu,Bw. Bakari Majid. Hafla hiyo ilifanyika makao
makuu ya Serengeti Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Droo ya kwanza ya kukuza mtaji, inayonjulikana kama “Tutokena Serengeti” imefanyika leo 25th/Nov/14
katika ofisi za Serengeti Breweries Chang’ombe ambapo Bi. Rukia
Athuman Almasi ameibuka mshindi wa kwanza wa Limo Bajaj.
Bi.
Rukia Athuman kutoka Morogoro alipokea taarifa hizi kwa mshituko na
bashasha baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa Limo Bajaji.
Akiongea kwa njia ya simu, Bi. Rukia Athuman Almasi alisema pamoja na
kushiriki promosheni hiyo hakujihesabu kama mwenye bahati kati ya wenye
bahati, hivyo basi ilimshangaza kuitwa mshindi.
Akiongea
na waandishi wa habari baada ya kumtangaza mshindi, Meneja chapa wa
bia ya Serengeti Premium Lager, Bwana. Rugambo Rodney alisema “SBL
inajivunia kwamba mashindano haya yamekuwa na mwanzo mzuri, shukrani kwa
ushirikiano kati ya Serengeti Breweries na B-Pesa. Droo hii ya kwanza
imeashiria kwamba kila mtu anaweza kushinda ili mradi tu ashiriki kwa
kunywa Serengeti Premium Lager”.
Kampeni
hii inatoa fursa kwa kila mtanzania aliye na umri wa miaka 18 na zaidi
kushiriki ambapo zaidi shilingi milioni 100 zinasubiri washindi na hii
ni fursa ambayo kila mtu hapaswi kuikosa.”.
Ili
kufanikisha kampeni hii, SBL imeungana na B-Pesa, wataalam wa
teknolojia mpya ambao hivi karibuni wamezindua mfumo mpya wa usafirihaji
wa fedha. B-Pesa watahusika pia katika kusambaza fedha kwa washindi
mbalimbali kote nchini kupitia simu za mkononi. Taarifa kutoka kwa
Mkurugenzi wa masoko wa B-Pesa, Mr. Salil Abbas zilisema kuwa “kampeni
imeanza vizuri na takwimu zinaonyesha kwamba watu wengi wameshiriki
zaidi katika kampeni hii zaidi ya matarajio yetu ya awali. Aliitaja
namba ya huduma kwa wateja ambayo ni 0225555000 ambayo itawasaidia
wateja ni jinsi gani wataweza kujichukulia zawadi zao pia kuelezea kwa
kina zaidi kwa wateja watakao kuwa na maswali.
“Tutoke
na Serengeti” ni kampeni inayowazawadia wateja zawadi murua ya utalii
wa ndani kwa kuwapeleka washindi kufurahia mwisho wa wiki na wapenzi
wao katika mbuga za taifa.
Kampeni
hii ninawalenga wateja zaidi ya milioni 20 walio katika nafasi ya
kushinda fedha taslim zenye thamani ya shilingi milioni 100 ambazo
zimegawanywa katika mafungu ya shilingi 5,000, pia kuna bajaji sita aina
ya Limo ambazo zinajulikana pia kama ‘Serengeti Bajaj’ zenye uwezo wa
kubeba abiria saba. . Pia kutakuwa na washindi wa bia za bure ambazo
zitakuwa zikipatikana katika baa nchi nzima.
Promosheni
hii ni kampeni ya kitaifa itakayoendeshwa kwa miezi mitatu. Ili kuwa
mshindi, unachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Serengeti Premium Lager
na kuangalia chini ya kizibo kujua kama umeshinda. Namba ya kodi ambayo
mteja atatumia baada ya kufungua kizibo ilitajwa kuwa ni 15317 na baada
ya hapo utaingizwa kwenye droo ya kujishindia zawadi mbalimbali
Post a Comment