Wachezaji wa Setif Entete washerehekea baada ya kuishinda As Vita ya DRC Congo
Kilabu
ya Entente Satif kutoka Algeria imeshinda ubingwa wa kilabu bora barani
Afrika kwa mara ya kwanza katika miaka 26 baada ya kuishinda kilabu ya
AS Vita Club kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana na mabao
ya ugenini kufuatia sare ya 3-3 siku ya jumamosi.
Raundi ya pili
ya fainali katika uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida ilikamilika kwa
sare ya 1-1,siku sita baada ya sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza
iliochezwa mjini Kinshasa.
Setif ilianza kuona lango na wapinzani
wao dakika nne katika kipindi cha pili kupitia Sofaine Younes ambaye
alifunga bao kupitia pasi ya El Hadi Belameiri.
Lakini wageni hao
walisawazisha dakika tano baadaye kupitia Lema mabidi aliyepiga mkwaju
kutoka nje ya eneo la kupigia penalti ili kuimarisha matumaini ya timu
yake.
Mabidi pia alikuwa ameifungia kilabu hiyo mabao yake mawili katika raundi ya kwanza ya mchuano huo wikendi iliopita.
Bao
hilo lilisababisha mechi hiyo kuwa ngumu ambapo Vita ilionyesha mchezo
mzuri ikilinganishwa na wapinzani wao Setif waliojaribu kutumia mbinu
chafu za kupoteza mda huku mashabiki wa kilabu hiyo wakitaka mchezo huo
kukamilishwa kuanzia dakika ya 75.
إرسال تعليق