SILAHA MSIKITINI

 

BAADHI ya vijana waliokamatwa ndani ya misikiti ya Musa na Sakina, eneo la Majengo, Mombasa, wakati wa msako wa polisi usiku wa kuamkia jana ambapo kijana aliuawa na washukiwa zaidi ya 251 kukamatwa.Silaha mbalimbali zikiwemo gruneti, bastola, visu na mapanga zilipatikana ndani ya misikiti hiyo. Picha/LABAN WALLOGA
KIJANA alipigwa risasi na kuuawa na wenzake zaidi ya 250 kukamatwa kwenye operesheni kali ya kusaka magaidi mjini Mombasa jana.

Maafisa wa polisi pia walipata silaha mbalimbali ndani DANIEL NYASSY na WACHIRA MWANGI ya misikiti ya Masjid Musa na Sakina. Misikiti hiyo ambayo inaaminika kuwa kumbi za kutoa mafunzo ya itikadi kali kwa vijana sasa imefungwa hadi operesheni hiyo itakapokamilika. Msako huo ulianza usiku wa manane na ulikuwa ukiendelea kufikia Silaha KUTOKA UK 1 jana jioni tukienda mitamboni.

Vijana 16 walikamatwa ndani ya msikiti wa Masjid Musa na wengine wanane wakapatikana kwenye msikiti wa Sakina.

Maafisa wa usalama walisema walipata vitanda, magodoro, mablanketi na mahali pa kupikia ndani ya misikiti hiyo ishara kwamba kuna watu ambao wamekuwa wakiishi humo.

Akihutubia wanahabari katika kituo cha polisi cha Urban, mjini Mombasa, afisa mkuu wa polisi (OCPD) Mahmoud Salim, alisema kijana aliyeuawa alijaribu kushamulia maafisa wa usalama kwa gruneti walipokuwa wakiingia msikitini.

“Walimpiga risasi kabla ya hajatupa gruneti hiyo na kumwua papo hapo,” akasema Bw Salim na kuapa kuwa operesheni hiyo itaendelea hadi wahalifu wote wanaswe.

Miongoni mwa vitu vilivyopatikana ndani ya misikiti hiyo ni ‘unga’ mweusi wa risasi unaotumiwa kutengeneza vilipuzi, gruneti sita, bastola mbili na risasi sita.

Kulikuwa pia na mapanga, visu, simu za mkononi, kanda za video, leseni za kuendesha gari, vitambulisho, vyeti vya tabia njema na vifaa vya kuhifadhia data za kielekroniki.

AL SHABAAB Vifaa vingine ni bendera nyeusi ambayo inafanana na ile ya kundi la kigaidi la Al Shabaab, darubini, mabegi, sanduku, kipakatalishi, nembo sita za polisi, misumari, laini za simu na nyundo. 
Polisi wanasema kanda za video zilizopatikana zimejaa mafunzo ya itikadi kali.

Zingine zina jumbe za kusifia waliokuwa wahubiri tatanishi wa kiislamu Sheikh Abdu Rogo na Sheikh Makaburi.

Baadhi ya kanda hizo zina maandishi haya: Jinsi ya kutumia bunduki aina ya AK-47, Majibu kwa wanaopinga Jihad, Sehemu zinazoogofya nchini Amerika, Masjid Musa Dahwa na Simba Jangwani.

“Tuliamua kufanya msako huo kufuatia msusuru wa visa vya uhalifu katika eneo la Mvita na taarifa za kijasusi ambazo zilionyesha kuna silaha kwenye misikiti ya Masjid Musa na Sakina,” akasema Bw Salim.

Wakati huohuo, viongozi wa eneo la Mombasa wametaka vijana waliotiwa mbaroni waachiliwa mara moja kama hawatapatikana na hatia.

Wakiongozwa na gavana Hassan Joho, viongozi hao walifika katika makao makuu ya polisi ya kaunti hiyo ambako walishauriana na maafisa wakuu wa polisi kwa karibu saa mbili.

Walishutumu maafisa wa polisi kwa kuvamia msikiti wakisema ni mahali patakatifu pa ibada.

Wengine walikuwa Seneta Hassan Omar, Mwakilishi wa Wanawake Mishi Juma Mboko na wabunge Abdulswamad Nassir (Mvita), Rashid Bedzimba (Kisauni) na Badi Twalib (Jomvu). 
- Taifa Leo

Post a Comment

Previous Post Next Post