Kama ni kweli basi nchi hii inahitaji maombi. Ikiwa bado
Tanzania inakabiliwa na skendo ya pembe za ndovu zinazodaiwa kuondoka na
ndege ya rais wa China alizuru nchini, kashfa nyingine kubwa imezuka!

Tanzania inashutumiwa kurejesha mpango wa kuwahamisha wamasai 40,000
katika eneo waliloishi kwa miaka na miaka, ili kuipa eneo hilo familia
ya kifalme ya Dubai kwaajili ya kuwinda wanyama.
Mwaka jana serikali ilidai kuahirisha mpango wa kutenga eneo la
square mita 1,500 zinazotengenisha mbuga ya wanyama ya Serengeti kwa
matumizi uwindaji wa biashara utakaofanywa na kampuni yenye makazi yake
kwenye falme za kiarabu, Ortelo Business Corporation (OBC).
Na sasa gazeti la The Guardian
na Uingereza na mengine, yameandika kuwa mpango huo umerejea na wamasai
hao wameamrishwa kulihama eneo hilo kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Wawakilishi wa wananchi hao wanakutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
bungeni Dodoma kuelezea hasira yao. Wanadai kuwa kuondolewa kwenye
ardhi hiyo ni kunyang’anywa kwa urithi wao na maisha ya watu 80,000
yataathirika. Eneo hilo ni muhimu kwa malisho ya mifugo ya wananchi hao
wanaoishi kwa kutegemea ufugaji.
Serikali itawalipa shilingi bilioni moja kama fidia ambazo wamasai wamezikataa.
“Nahisi kusalitiwa,” mratibu wa kikundi cha Ngonett Samwel Nangiria ameliambia The Guardian.
“Bilioni moja ni ndogo saba huwezi kulinganisha na ardhi. Imerithiwa. Mama na bibi zao wamezikwa kwenye ardhi ile. Hakuna cha kulinganisha nayo.”
“Bilioni moja ni ndogo saba huwezi kulinganisha na ardhi. Imerithiwa. Mama na bibi zao wamezikwa kwenye ardhi ile. Hakuna cha kulinganisha nayo.”
Msemaji wa wizara ya Maliasili na Utalii, ameliambia gazeti hilo kuwa
hana taarifa kuhusiana na mpango huo. Habari hiyo imeandikwa Jumatatu
kwenye magazeti na vyombo vingi vikubwa vya habari duniani likiwemo Daily Mail, rt.com ya Urusi, eTurboNews, The Week Uk, Europa Press, Ecoblog.it na vingine.
إرسال تعليق