\
Picha ya Kopyuta ikionyesha athari za Alzheimer
Tatizo
la kukosa usingizi huenda likawa ishara ya kutambua
mapema maradhi ya kupiswa na akili au ''Alzheimer'' kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa kwa kutumia panya ambaye ana
maumbile yanayofananishwa na binadamu.
Vipande
vya protini, kwa lugha ya kitaalamu (plaques) au utando
kwenye ubongo yanadhaniwa kuwa sehemu nyeti
inayosababisha maradhi haya.
Utafiti
uliofanywa na kuchapishwa katika jarida la tafsiri ya
matukio ya Sayansi, umeonyesha kuwa punde chembe chembe
za utando ule ulipoanza kumea kwenye ubongo wa panya,
usingizi ukaanza kuwa tatizo kwa viumbe hao.
Taasisi
inayosimamia utafiti wa maradhi hayo, (Alzheimer's
Research UK) imehimiza kuwa ikiwa uhusiano huo unaweza
kuthibitishwa huenda ikawa muhimu kwa Madaktari.
Utafiti
wa kutaka kugundua mapema kama mtu anaelea kukumbwa na
maradhi ya Alzheimer inadhaniwa kuwa muhimu katika kutibu
maradhi hayo.
Mgonjwa wa kupiswa na akili
Wagonjwa
hawaonyeshi dalili kupitia hisia au kumbukumbu zao hadi
baada ya mda mrefu wa maradhi kumkumba mgonjwa.
Yanapofikia hapa sehemu za ubongo huwa zimeharibika kiasi
kwamba tiba inakua vugumu kupatikana au hata kushindwa kupatikana.
Ndiyo
sababu wataalamu wanafanya juhudi za kuanza mapema
kugundua kama mtu atapata maradhi haya, miaka kadhaa
kabla ya dalili hizo kujitokeza.
Viwango
vya protini ijulikanayo kama beta amyloid kimaumbile
hupanda na kushuka miongoni mwa binadamu na pia panya
katika kipindi cha saa 24. Hata hivyo ni ile protini
ambayo husababisha utando usiofutika kwenye ubongo na
maradhi ya Alzheimer.
Majaribio
yaliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Washington
yameonyesha kuwa panya wanaotoka usiku kwa kawaida hulala
kwa dakika 40 kwa kila saa mchana. Lakini ubongo
ulipoanza kupatwa na uchafu panya hawa wakaanza kusinzia
kwa dakika 30 pekee.
Mmojapo
wa wataalamu, Prof David Holtzman, alisema: "endapo
mapungufu katika usingizi huanza mapema kiasi hiki katika
ugonjwa wa Alzheimer, mabadiliko hayo yanaweza kutupa
ishara ya wepesi wa kuweza kuyatambua maradhi haya."
Utando kwenye ubongo
"ikiwa
matatizo haya ya usingizi yapo, hatuelewi hasa
yanachukua mfumo gani, kupungua kwa usingizi kikamilifu
au ni tatizo la kushindwa kabisa kulala au ni kitu
tofauti kabisa."
Hata
hivyo, utafiti unaofanyika kwa kutumia panya mara nyingi
hayafai kutumika kwa binadamu kwa sababu nyingi
zinzosababisha kutatizika na usingizi.
Dr
Marie Janson, kutoka shirika la kujitolea Alzheimer's
Research UK, ametaka utafiti zaidi ufanywe kwa kuwapima
binadamu kuona kama kuna uhusiano baina ya matatizo ya
kukosa usingizi na ugonjwa wa Alzheimer.
Aliongezea
kuwa: "tayari umekuepo utafiti unaounganisha mabadiliko
katika usingizi huchangia katika matumizi ya ubongo kwa
fikra, lakini matokeo haya yanaonyesha kuwa kuna
uwezekano kwamba mapungufu katika usingizi pia inaweza
kuwa ishara na onyo la maradhi ya kusahau
Post a Comment