![]() |
| Jua linavyoonekana kupitia nkamera ya Soho |
TEKNOLOJIA iliyoanzia enzi za zama za mawe inatumika kujenga chombo cha anga za juu ambacho kitatumwa kupeleleza jua, chanzo cha nishati ya dunia.
Teknolojia hiyo ni kutumia vumbi la mifupa ya wanyama waliokufa.
Chombo hicho kinatumwa kulichunguza jua kwa ukaribu zaidi.
Kazi ya kutengeneza chombo hicho inafanyika kwenye taasisi ya Airbus Defence and Space iliyoko Stevenage kaskazini mwa London, nchini Uingereza.
Mtaalamu anayeshughulika na suala hilo, Chris Draper , amesema kwamba ingawa ukitazama vifaa vinavyofanyiwa majaribio unaweza kuona kana kwamba ni vitu vya kawaida,hata hivyo vifaa hivyo vina asili ya mifupa ya wanyama waliokufa.
Mifupa hiyo kwa mujibu wa Draper ndiyo inayotengeneza ukanda wa kukabili joto. Ukanda huo wa kukabili joto wenye unene wa milimita 1/20,ulio katika foili la titanium ni muhimu katika kuhakikisha kwamba chombo hicho kinafika salama katika eneo linalotakiwa na kuendelea kufanyakazi iliyokusudiwa.
Chombo hicho ambacho kinatarajiwa kurushwa mwaka 2017 kinachotumwa na Taasisi ya Utafiti wa anga za juu Ulaya (ESA) kwenda kupeleleza jua kinatarajiwa kuzunguka jua katika umbali wa kilomita milioni 40, ikiwa ni karibu zaidi na nyota iliyo karibu yetu; huku ikiwa ndani ya mzingo wa sayari ya Mercury.
Chombo hicho kinatarajiwa kuleta taarifa nyingi kuhusu mwenendo wa jua na nishati yake ya kiwango cha juu inayomwaga katika mfumo wa jua ambazo sayari 10 zinawezeshwa nguvu za mvutano kutoka kwake huku ikitoa uhai katika sayari ya dunia, katika kuangalia majira na nyakati.
Aidha itachunguza namna inavyoiwezesha dunia na teknolojia ya mifumo ya setelaiti ambayo inategemewa sana duniani kwa ajili ya shughuli mbalimbali pamoja na kujihami na majanga yanayoweza kuikabili dunia kutoka sayari nyingine.
![]() |
| taswira itakavyokuwa |
Ili chombo hicho kiweze kufanyakazi yake kinatakiwa kiweze kuhimili joto la digrii 550 selisius kwa upande unaotazama jua na ule usiotazama jua joto hasi la digrii 200, huku vifaa vyake vya kazi na vile vya kielektroniki na vinavyotoa msukumo wa safari kufanyakazi bila athari.
Mtaalamu huyo katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) amesema kupata zana zinazoweza kusaidia vifaa visiyeyushwe na joto kali si rahisi kwani walilazimika kujiuliza ni aina gani ya mali ghafi inaweza kusaidia kazi hiyo.
Ukanda huo wa kuzuia joto wenye unene wa mita 3.1m-kwa-2.4 unatakiwa kuwa mwepesi ili kuwezesha roketi kukiondoa chombo hicho duniani na kuhimili miaka mitano ya safari ikikumbana na mambo mbalimbali angani.Aidha ngao hiyo ni lazima iwe na vipenyo vitakavyowezesha kufunga na kufunguka kuwezesha mitambo iliyomo ndani ya kisayansi kuchukua takwimu muhimu za Jua na kurejesha duniani.
Ngao dhidi ya jua inatarajiwa kuwa na kanda 18.
Titanium ni aina ya metali ambayo imechaguliwa kutokana na nguvu ytake ya kuhimili joto la mpaka sentigredi 1,668 lakini kuwepo kwa ukanda wa rangi nyeusi kumetokana na nadharia ya kawaida ya sayansi kwamba pamoja na titanium kuwa na uwezo wa kurejesha mwanga inahitaji rangi nyeusi ya kutoa joto ndani.
Lojiki inaonesha kwamba unaposafiri karibu na jua,rangi nyeupe itakuwa inarejesha sehemu kubwa ya mwanga na hivyo kuzuia joto jingi lakini upo ukweli kuwa ukanda mweuepe hautoi joto nje kama ilivyo kuwa rangi nyeusi.
Utafiti wa wataalamu ndio ulioonesha haja ya chombo hicho kuwa na ukanda mweusi ili kutoa joto kwenye anga za juu, tatizo likawa ni aina gani inaweza kukaa kuhimili joto na kutobadilika wala kumeguka na ndio wakaja na teknolojia hiyo ya zamani.
Binadamu wametumia mifupa ya wanyama kutengeneza rangi ambazo zimetumika kuchora katika miamba toka zamani, na kanuni iliyotumika ni ilke ambayo hadi sasa wanasayansi wlaitumia, kuyeyusha.
Mifupa hiyo inaunguzwa hadi kupatikana kwa rangi nyeusi kama ile ya mkaa, pamoja na ukweli kwamba ni teknolojia ya zamani sana lakini ndio hasa yenye uwezo wa kile kinachotakiwa anga za juu.
Majaribio ya uvumilivu wake katika joto kali na baridi kali yameonesha kwamba mifupa hii ambayo ni teknolojia ya zamani inafaa kabisa kutumika kwa shughuli za kisasa.


إرسال تعليق