JOTO la uchaguzi likiwa likizidi kupanda kila
kukicha Mbunge wa Mpwapwa Gregory Teu (CCM) ameulalamikia uongozi
wa chama hicho kwa kufumbia macho vitendo vibaya vinavyo endelea
dhidi yake.
Amedai kuwa kaanza kukashifiwa na kutukanwa na baadhi ya mawakala walioonyesha nia kugombea ubunge mwakani 2015 mbele ya viongozi wa chama cha wakati muda wa kampeni haujafika huku viongozi hao wakilifumbia macho vitendo hivyo.
Teu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake mjini hapa juu ya kampeni chafu zinazoendelea dhidi yake wakati muda wa kampeni haujafika.
Alisema kuwa “baadhi ya watu walionyesha nia ya kuja kugombea mpwapwa.Wamekuwa wakiwatumia vijana ambao naweza kuwaita wahuni kila asubuhi wakipita na spika mitaani kwa kunitolea maneno ya kashifa ambayo mengine ni kuhusu mimi na familia yangu na ubunge wangu na viongozi wangu wa chama wakiliangalia swala hili bila kuchukulia hatua za kinidhamu” aliongea.
Alisema kampeni hazijaanza ila tunaona bila kificho, kujificha baadhi ya watu wamekuwa wakienda vijijini na kutengeneza baadhi matisheti kama Nanga inapaa ambazo ni kampeni na kunipaka matope kwa wapiga kura kitu ambachoalikisema kuwa kinaweza kukigawa chama Teu amedai kuwa kauli wanazo zitoa kwa wapiga kura kuwahajafanya chohote katika ahadi zimekuwa zikaminiwa na wananchi wachache aliowanunua kufanya kampeni na wengine wasio weza kufanya uchambuzi wa kina.
Alisema katika ahadi zake alizo kuwa ameahidi kwa kwawananchi
zimetekelezeka kwa asilimia zaidi ya 75% ikiwemo barabara ya lami 1km kusambaza
umeme vijijini ambayo ni mradi wa wakala wa samabaji wa ememe vijijini LEA na
matengenezo ujenzi wa shule ya msingi chunyu B na alisema kuwa anategeme
kujenga miradi ya mawasiliano katia kata ya matomondo na mima ili kurahisha
mawasiliano.
Pia alidai majina hayo ameyapeleke kwa kamati ya maadili ya siasa na kumuonya mjumbe huyo lakini viongozi wa chama kuendelea kuyafumbia macho matendo hayo kiyu alicho dai kuwa kuna baadhi ya viongozi wa chama kwa kuwapoza kwa kitu kidogo.
Teu alisema kuwabaadhi ya wagombea wamekuwa wakiwalaumiwa baadhi ya viongozi wa chama kuwawekea bili ya pombe baadhi ya baa hapa wilayani na kusababisha viongozi hao kupigana wakiwa baa baada ya kudhulumiana mgao iliokuwa umetumiwa kwa muonyesha nia mmoja.
Aidha amedai kuwa “kuna mjina mengi yaliotangaza nia ya kuwania ubunge wa Mpwapwa lakini sijawalalamikia huyu kuziganika na kundi lake ananichafua ndio maana nimeamua kulizungumzia suala hili”alisema Teu .
Akijibu tuhuma hizo katibu wa chama cha mapinduzi (CCM)
wilayani hapa Ndaluone Mbogo amekanusha kuwa kampeni hizo bado hazijaanza na
wale hawajasikia popote “kama mtu analalamika alete barua ya maandishi tuya
shughulikie kiofisi aliseme” Mbogo.
Alidai kuwa baadhi ya walionyesha nia wakifanya hivyo ni kukiuka taratibu za chama na kukichafua chama.
Alipo ulizwa juu ya tuhuma za kuwekewa bili ya pombe na kupigana baadhi ya waonyesha nia alikanusha na alisema hizo ni siasa za kuchafuana katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Pia alisema kuna vijana wanaopita na maspika na kumnadi baadhi ya mjumbe aliyeonyesha nia na kasema suala hilo wamelifikisha polisi, na kijana huyo anaupungufu wa akili
“ Yule yohane mapilau ndo anapita
na spika ila Yule anacheti cha milembe Yule na
alipelekwa polisi mala kadhaa lakini hajaacha alifaanua
Ndauluone.
mwisho
Post a Comment