Teu alia rafu jimboni kwake



 
JOTO la uchaguzi likiwa  likizidi kupanda  kila kukicha  Mbunge wa Mpwapwa Gregory Teu (CCM) ameulalamikia uongozi wa  chama hicho kwa kufumbia macho  vitendo vibaya vinavyo endelea dhidi yake.

Amedai kuwa kaanza kukashifiwa na kutukanwa na baadhi ya mawakala walioonyesha  nia kugombea ubunge mwakani 2015 mbele ya viongozi wa chama cha wakati muda wa kampeni haujafika huku viongozi hao wakilifumbia macho vitendo hivyo.

Teu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake mjini hapa  juu ya kampeni chafu zinazoendelea dhidi yake wakati muda wa kampeni haujafika.

Alisema kuwa “baadhi ya watu walionyesha nia ya kuja kugombea mpwapwa.Wamekuwa wakiwatumia vijana ambao naweza kuwaita wahuni kila asubuhi wakipita na spika mitaani kwa kunitolea maneno ya kashifa ambayo mengine ni kuhusu mimi na familia yangu na ubunge wangu na viongozi wangu wa chama wakiliangalia swala hili bila kuchukulia hatua za kinidhamu” aliongea.

Alisema kampeni hazijaanza ila tunaona bila kificho, kujificha baadhi ya watu wamekuwa wakienda vijijini na kutengeneza baadhi matisheti kama Nanga inapaa ambazo ni kampeni na kunipaka  matope  kwa wapiga kura kitu ambachoalikisema kuwa kinaweza kukigawa chama Teu amedai kuwa kauli wanazo zitoa kwa wapiga kura kuwahajafanya chohote  katika ahadi zimekuwa zikaminiwa na wananchi wachache aliowanunua kufanya kampeni na wengine wasio weza kufanya uchambuzi wa kina.

Alisema katika ahadi zake alizo kuwa ameahidi kwa kwawananchi zimetekelezeka kwa asilimia zaidi ya 75% ikiwemo barabara ya lami 1km kusambaza umeme vijijini ambayo ni mradi wa wakala wa samabaji wa ememe vijijini LEA na matengenezo ujenzi wa shule ya msingi chunyu B na  alisema kuwa anategeme kujenga miradi ya mawasiliano katia kata ya matomondo na mima ili kurahisha mawasiliano.

Pia alidai majina hayo ameyapeleke kwa kamati ya maadili ya siasa na kumuonya mjumbe huyo lakini viongozi wa chama kuendelea kuyafumbia macho matendo hayo   kiyu alicho dai  kuwa kuna baadhi ya viongozi wa chama kwa kuwapoza kwa kitu kidogo.

 Teu alisema kuwabaadhi ya wagombea wamekuwa wakiwalaumiwa baadhi ya viongozi wa chama kuwawekea bili ya pombe baadhi ya baa hapa wilayani na kusababisha viongozi hao kupigana wakiwa baa baada ya kudhulumiana mgao iliokuwa umetumiwa kwa muonyesha nia mmoja.

Aidha amedai kuwa “kuna mjina mengi yaliotangaza nia ya kuwania ubunge wa Mpwapwa lakini sijawalalamikia huyu kuziganika na kundi lake ananichafua  ndio maana nimeamua kulizungumzia suala hili”alisema Teu .

Akijibu tuhuma hizo katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani hapa Ndaluone Mbogo amekanusha kuwa kampeni hizo bado hazijaanza na wale hawajasikia popote “kama mtu analalamika alete barua ya maandishi tuya shughulikie kiofisi aliseme” Mbogo.

Alidai kuwa baadhi ya walionyesha nia wakifanya hivyo ni kukiuka taratibu za chama na kukichafua chama.

Alipo ulizwa juu ya tuhuma za kuwekewa bili ya pombe na kupigana baadhi ya waonyesha nia  alikanusha na alisema hizo ni siasa za kuchafuana katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu.
Pia alisema kuna vijana wanaopita na maspika na kumnadi baadhi  ya mjumbe aliyeonyesha nia na kasema suala hilo wamelifikisha polisi, na kijana huyo anaupungufu wa akili

“ Yule yohane mapilau  ndo   anapita  na  spika  ila Yule  anacheti cha milembe  Yule na alipelekwa polisi   mala kadhaa lakini hajaacha alifaanua  Ndauluone.
mwisho

Post a Comment

أحدث أقدم