Tucta yamtaka JK kuwatimua waliohusika kuchota Escrow

Rais wa Tucta,Gratian Mukoba.
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limemtaka Rais Jakaya Kikwete atumie rungu lake kuwawajibisha vigogo  wote waliohusika na uchotaji wa fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, liyoko katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). 
Rais wa Tucta, Gratian Mukoba, (pichani) aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Alisema Tucta inaamini kuwa wizi kama huo wa fedha za umma unakwamisha jitihada za  kupatikana kwa mishahara bora kwa wafanyakazi pia unakwamisha ulipaji wa madeni ya walimu kwa muda mrefu.

“Tunajua kuwa zipo juhudi za kufunika suala hilo kupitia baadhi ya wabunge wanaojali maslahi yao, kamwe Tucta hatutakubali pamoja na Watanzania wanyonge kushuhudia fedha na rasilimali zikiibwa na kunufaisha wachache,” alisema.

Alisema wizi huo ni ishara kuwa nchi inaelekea kubaya kwani Watanzania wanyonge wamechoka kushuhudia rasilimali na fedha zikiendelea kuwanufaisha watu wachache huku kundi kubwa likiendelea kutaabika.
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

أحدث أقدم