Novemba 4, viongozi wakuu wa vyama vya Nation
League for Democracy (NLD), NCCR Mageuzi, CUF na Chadema walitiliana
saini ushirikiano wa kusimamisha mgombea mmoja kila ngazi ya uchaguzi
kuanzia serikali za mitaa, vijiji na vitongoji. Kusambaratika kwa umoja
huo kulitokana na viongozi wa vyama vya CUF, NCCR Mageuzi na Chadema
kukaa vikao vitatu kupanga jinsi ya kuachiana vijiji, vitongoji na mitaa
kushindikana kufuatia viongozi wa Chadema kuvitaka vyama vingine
kuwaachia vitongoji 24 vya Mamlaka ya Mji Mdogo Mugumu.
Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Serengeti, Joseph
Magoiga alisema Mamlaka ya Mji Mdogo wana vitongoji vinne na Chadema
kimoja kati ya 23, wamesimamisha wagombea tisa na NCCR-Mageuzi wawili na
kuwaachia Chadema 12.
“Vigezo vya makubaliano yaliyotiwa saini ni kuwa
na mgombea anayekubalika… Wao wanataka vitongoji vyote ili wakishinda
washike mamlaka ya mji, tunapoomba vigezo vya wao kutaka vitongoji vyote
hadi tunavyotetea wanasema wao ndiyo wanaokubalika,” alisema Magoiga.
Novemba 15, viongozi hao walikutana ofisi ya
Shirika la Kusaidia Watoto Yatima kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 6:00,
Novemba 16 walikutana ofisi ya CUF Wilaya na kikao cha mwisho walikutana
nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa vyama hivyo bila kupata mwafaka.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Wilaya ya Serengeti,
Tano Mwita alisema wapo tayari kuwania vitongoji viwili na Chadema
kuachiwa 12 lakini hawataki.
“Wanadai waraka waliopewa na viongozi wao wa
ushirikiano ni tofauti na tulionao vyama vingine… ulipowataka watusomee
au wauonyeshe wakadai upo kwenye simu, tumewajulisha viongozi wa juu wa
vyama vyetu kuwa ushirikiano huu una walakini,” alisema.
Katibu wa Chadema Wilaya, Julius Anthony alisema
wamesimamisha wagombea 21 kati ya 23 na kwamba, wamewaachia NCCR Mageuzi
na CUF kwani wamefikia hapo baada ya vyama hivyo kushindwa
kuwathibitishia jinsi wanavyokubalika.
“Hata sekretarieti ya chama mkoa waliafiki kila
chama kipambane pekee, kuna vijiji ambavyo tumekiachia NCCR Mageuzi
kwani hatuna nguvu… tulizingatia mwongozo kwa kuja na wajumbe wa matawi
ili tuweze kupiga kura,” alisema Anthony na kuongeza:
“Wenzetu hawakuwa na wajumbe ikawa ndiyo mwanzo wa kila mmoja kufanya anavyojua.”
Makubaliano ya Ukawa ni marufuku chama kilichopo
kwenye ushirikiano kuchukua wanachama, kutumia mwafaka na mashauriano,
kuwashindanisha wagombea kwa sifa na kazi zote kuratibiwa na ngazi ya
wilaya.
Post a Comment