Uturuki yathamini wanawake zaidi



Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan
Raisi wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan,ametoa kauli kuwa wanawake hawako sawa na wanaume kutokana na tofauti zao za kimaumbile.
Bwana Edogan,ambaye ni mcha Mungu na hafidhina wa dini ya kiislam,ametoa kauli hiyo mbele ya mkutano mkubwa wa wanawake mjini Istanbul , na kusema kwamba wanawake wajawazito ama wanawake wazazi, hawapaswi kuyoka nje ya nyumba zao kulima,na waislam wanawatambua wanawake kuwa ni wazazi.
Kutokana na kauli hiyo Raisi Edogan amesema bayani kuwa wanaharakati hawatamuelewa.Mwandishi wa bbc nchini Uturuki ameeleza kauli ya raisi huyo ni kama yenye kutaka kukata rufaa kwa waungaji mkono wake na waswalihinna lakini wengi wao wanaiangazia dunia zaidi badala ya uhuru wa Taifa hilo.
Bwana Edogan hivi karibuni alitoa kauli kuwa kila mwanamke nchini humo anapaswa kuwa na watoto watatu tu, na kupendekeza judhibiti haki ya utoaji mimba.BBC

Post a Comment

أحدث أقدم