Katika gazeti hili toleo namba 1151 la Septemba 27-30, 2014 kulikuwa na
habari iliyokuwa na kichwa kisemacho; ‘UGAIDI BONGO’ AL-SHABAAB
WATAKAVYOTUMIA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA KUTEKA NDEGE.
Uwanja wa ndege wa Mwanza.Hata hivyo, licha ya habari hiyo kuonyesha mazingira ambayo si salama na kuitaka mamlaka ya viwanja vya ndege nchini kuchukua hatua, hakuna kilichofanyika na inaonesha hali ya usalama ya uwanja huo ni sikio la kufa.
Mwandishi wetu alipotembelea hivi karibuni eneo lenye mlango huo uliopo kwenye jengo linalotazamana na maegesho ya magari karibu na mlango wa VIP alikuta liko vilevile.
Mlango
huo wa kioo uliopo kwenye jengo jipya la kusubiri abiria kupanda ndege,
umeandikwa ‘EXIT’ ukimaanisha ni wa kutokea wakati wa dharura hivyo mtu
mwenye nia mbaya anaweza kuufikia na kuutumia kwa uhalifu.Kwa mara nyingine tena tunaukumbusha uongozi wa uwanja huo kuchukua tahadhari kabla ya hatari kwa kuhakikisha wanauziba mlango huo ambao unaweza kutumiwa na magaidi.
Aidha, Risasi Jumamosi linaendelea na jitihada za kumtafuta Waziri wa Uchukuzi, Harrison George Mwakyembe ili kumfikishia suala hilo na kuona namna anavyoweza kuhakikisha linafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
Post a Comment