UZINDUZI
wa filamu ya Wape Salamu Zao unatarajia kufanyika siku ya Jumapili
tarehe 9 November katika ukumbi Travetine Magomeni, jijini Dar es
salaam.
Uzinduzi
huo utambatana na ujio wa sesson 2 kipindi cha Ulimwenguni wa filamu
cha TBC 1,kinachoongozwa na Juma Mtetwa katika, kivutio kikubwa ni
Jackson Kabirigi ‘Kisate’.
“Nimepanga
kuacha historia katika uzinduzi wa filamu ya Wape Salamu Zao, kuna vitu
vingi sana ambavyo sijawahi kuwaonyesha watazamaji hajawahi kuviona
kutoka kwangu tarajieni maajabu,”anasema Kabirigi.
Uzinduzi
huu unasindikizwa na gwiji la muziki wa Taarab Bongo mfalme Mzee Yusuf,
ambaye naye ameahidi kufanya show ya kipekee haijawahi kutokea hivi
karibuni, na kuimba nyimbo zinazotamba na kufanya vizuri Tanzania.
Wasanii
nyota wa filamu kutoka Bongo movie watakuwepo wakiwa wamependeza huku
zuria jekundu likipamba sehemu ambayo watu watapata nafasi ya kupiga
piga katika mapozi, show hiyo ya kufunga mwaka kiingilio ni 8,000/ tu
kwa mtu mmoja si ya kukosa.
.jpg)
.jpg)
Post a Comment