Mkuu
wa majeshi nchini Jenerali Davis Mwamunyange amewataka vijana
wanaomaliza mafunzo ya jeshi na kukosa nafasi za ajira kutumia mafunzo
mbalimbali wanayoyapata JKT hasa ya stadi za kazi kuelimisha wengine
ikiwa ni pamoja na kudumisha amani katika maeneo wanayoishi.
Jenerali Mwamunyange ametoa wito huo jijini Dar es Salaam wakati wa
gwaride maalum la kuwaaga majenerali wastaafu zoezi lililofanyika
viwanja vya kambi ya twalipo mgulani ambapo amesema vijana wanapoingia
jeshini mbali na kupewa mafunzo ya kijeshi lakini pia wanapata mafunzo
mbalimbali ikiwemo ufugaji, kilimo, ufundi wa aina mbalimbali ili
wanapohitimu waweze kujitegemea huku wakiwataka maofisa wengine kufuata
nyao za waliostaafu.
Kwa upande wao baadhi ya majenerali waliostaafu wamesema kwa sasa
jeshi limepiga hatua kiteknolojia tofauti na wao walivyojiunga na jeshi
na kuongeza kuwa ni bora kuwa na jeshi dogo lakini la kitaalam huku
wakiwataka wanaoandikisha vijana kuingia jeshini kuhakikisha wanakuwa
waadilifu wakati wa kuchuja ili kupata vijana wenye vigezo.
Sherehe hizo zimepambwa na mazoezi mbalimbali likiwemo gwaride
maalum la kuwaaga wastaafu hao pamoja na zoezi la wao kukabidhi
vitambulisho vyao vya kazi kwa mkuu wa majeshi na yeye kuwakabidhi
vitambulisho vya kwenda uraiani pamoja na funguo za gari ambayo
yametolewa na jeshi baada ya kulitumikia kwa kwa uadilifu muda wote huo
- ITV
- ITV
KAULI YA WAZIRI MEMBE
BUNGENI KUHUSU BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA NDOVU.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe
Mheshimiwa Spika,
Siku ya Jana Vyombo vya Habari mbalimbali vya Ndani na Nje ya Nchi
vilitoa habari kwamba ujumbe wa Rais wa China uliokuja nchini Miezi 18
iliyopita ulijihusisha na ununuzi wa pembe za ndovu nchini. Chanzo cha
habari hizo ni taarifa ya taasisi isiyo ya kiserikali ya nchini Marekani
ijulikanayo kama Environmental Investigation Agency (EIA). Habari hiyo
imekwenda mbali zaidi kuituhumu nchi yetu na viongozi wake kutojali,
wala kushughulikia tatizo la biashara haramu ya pembe za ndovu.
Mheshimiwa Spika,
Ninapenda kupitia Bunge lako tukufu kuutaarifu umma wa watanzania na
dunia kwa ujumla kwamba madai yaliyotolewa na NGO hiyo ya Marekani ya
kuihusisha ziara ya kihistoria ya Rais wa China kutembelea Tanzania kama
nchi ya kwanza toka aingie madarakani na biashara ya pembe za ndovu
hayana ukweli wowote. Vilevile, madai ya kwamba Serikali ya Tanzania
haijali na wala haichukui hatua dhidi ya wanaojishughulisha na biashara
haramu ya pembe za ndovu sio kweli.
Taarifa za EIA ni za kupikwa na kuungwa kuungwa ili kuchafua heshima ya
nchi yetu, pamoja na kuchafua heshima ya rafiki zetu Taifa la China. Ni
taarifa iliyoandaliwa na kutolewa wakati huu ili kukidhi ajenda mahususi
ambayo tunaifahamu fika.
Mheshimiwa Spika,
Kabla sijaelezea kwanini ninasema taarifa hii sio ya kweli ningependa
kwanza kulielezea Bunge lako tukufu mambo sita yafuatayo ambayo hayana
ubishi:
1) Moja, ni kweli soko kubwa la pembe za ndovu lipo China. Wanaofanya
biashara haramu ya pembe za ndovu hutafuta soko China;
2) Ni ukweli usiopingika kwamba pembe za ndovu nyingi zinazouzwa kwenye
masoko haramu zinatokea Afrika, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi
zinapotoka pembe hizo;
3) Biashara hiyo haramu inahusisha wahalifu/ na mitandao ya waalifu
ambao wana uraia wa nchi mbalimbali zikiwemo China na Tanzania;
4) Serikali ya Tanzania na Serikali ya China hazifanyi biashara haramu
ya pembe za ndovu na wala hazihusiki na mitandao haramu.
5) Kwa kutambua ukubwa wa Tatizo la biashara hiyo haramu, Serikali zetu
mbili zimekuwa na ushirikiano wa karibu kabisa katika kukabiliana na
mitandao inayofanya biashara hiyo haramu. Vyombo vya dola vya nchi zetu
mbili vimeshirikiana kwa karibu na kupashana habari kila wakati
zilizowezesha kuwakamata wahusika wa biashara hiyo. Isitoshe wakati wa
ziara iliyomalizika hivi majuzi Serikali zetu mbili zilisaini mkataba wa
kutupatia vifaa vya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili wa
wanyamapori – (China Aided Equipment for Forest Resources and Wildlife
Conservation). Vilevile kwenye ziara hiyo tulisaini Mkataba wa kutupatia
mitambo ya kisasa ya kufanya ukaguzi wa mizigo bandarini- ambayo
itasaidia kubaini mizigo inayosafirishwa.
6) Tanzania na China zilishiriki kikamilifu kwenye Mkutano wa Kimataifa
wa Kudhibiti Biashara Haramu ya Pembe za ndovu (London Confrrence on
Illegal Wildlife Trade) uliofanyika mwezi Februari 2014. Moja ya
mafanikio makubwa ya mkutano huo ni kwa nchi za China, Botswana na
Tanzania kusaini mkataba wa kupambana na biashara hiyo haramu. Hii
ilikuwa ni mara ya kwanza kwa China kusaini Mkataba wa aina hiyo, jambo
linalodhihirisha umakini wa Serikali ya Rais Xi Jinping kushughulikia
tatizo la biashara haramu. Vilevile kabla ya mkutano huo wa London,
Serikali ya China ilichoma moto hadharani shehena ya meno ya tembo
haramu yaliyokuwa yakishikiliwa nchini humo.
Mheshimiwa Spika,
Baada ya kusema hayo, naomba sasa nitoe sababu kwanini ninasema habari
za NGO ya EIA ni za uongo;
Mheshimiwa Spika,
Taarifa kama hii iliyotoka kwenye New York times sio mara ya kwanza
kutolewa. Taarifa ya aina hii iliwahi kutolewa mwaka jana. Mtoa taarifa
ambaye ametajwa kuwa chanzo cha habari ni mtu mmoja ambaye walimkuta
barabarani na kuanza kumuuliza maswali. Mtu huyo sio mtumishi wa bandari
wala uwanja wa ndege. Ni mpita njia tu wa mtaani. Hata video ya
mahojiano inaonyesha hivyo. Ukiachilia mbali uwongo uliotolewa na bwana
huyo, taasisi ya EIA imeongelea tukio la kontena lililokamatwa Bandarini
likiwa na pembe za ndovu.
Ni kweli kabisa kwamba kontena la pembe lilikamatwa bandarini na vyombo
vya dola. Jambo moja ambalo watu wengi hawalijui ni kwamba mafanikio ya
operesheni ile yalitokana na ushirikiano wa vyombo vya usalama vya
Tanzania na China. Taarifa za kiinteligensia juu ya operation hiyo
zilitoka China na kuwasilishwa Tanzania ndio operesheni ikafanikiwa.
Lakini habari zilizotoka kwenye mitandao zilisema kwamba Kontena
limekamatwa likipelekwa kwenye meli ya kijeshi ya China...jambo ambalo
sio kweli.
Mbali na hayo, ziara ha Rais Xi nchini ilikuwa ya masaa 24, na programu
yake ilianza mara tu alipowasili nchini kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 4
usiku kwenye dhifa ya taifa. Siku ya pili ratiba ilianza asubuhi kwa
uzunduzi wa Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Baada ya hapo Rais Xi na Ujumbe wake walikuwa na mikutano na Rais wa
Zanzibar Mhe Dk.Ali Mohamed Shein na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe
Benjamin William Mkapa. Baada ya hapo Rais Xi na ujumbe wake walienda
kwenye makaburi ya Wachina kule Majohe na kisha wakaondoka kwenda uwanja
wa ndege. Sasa hizo shopping zinazoelezewa kufanywa na ujumbe wa rais
Xi zilifanyika saa ngapi?
Jambommuhimu kujiuliza, je hiyo taarifa ya Rais Xi na ujumbe wake kubeba
pembe za ndovu iweje itoke leo? Kwanini wakati huu baada ya ziara ya
Rais wetu nchini China? Kwanini itoke baada ya Mhe Rais kuhutubia
mafanikio ya ziara yake nchini China?
Mheshimiwa Spika,
Jibu kila mmoja anaweza kujua. Wasambazaji wa taarifa hizi hawaitakii
mema nchi yetu. Hawawatakii mema marafiki zetu wa China. Wamejawa na
wivu na husuda kwa mafanikio ya China. Inashangaza kuona, wanawachukia
huku wanawategemea. Wao wangependa wao peke yao wafanye biashara na
China, wakachukue mikopo China, wavutie uwekezaji kutoka China, lakini
tukifanya sisi waafrika inakuwa nongwa. Tusikubali upuuzi wa aina hii.
Sisi ni taifa huru, hatutachaguliwa marafiki wala hatutarisishwa maadui.
Tutaendeleza ushirikiano wetu wa kidugu na China na wala hatutorudi
nyuma kamwe kutoka na maneno ya uwongo na uzushi.
Aidha, ninapenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu Mheshimiwa Spika
kwamba Serikali yetu haitorudi nyuma. Tutaendeleza mapambano dhidi ya
biashara haramu ya pembe za ndovu. Wale wote wanaoshughulika na biashara
hizo, siku zao zimefikia mwisho.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Make money by copying the best: http://bit.ly/best_tips

إرسال تعليق