![](http://www.itv.co.tz/media/image/mauaji%282%29.jpg)
Watu
wanne wanao sadikiwa kuwa wezi wa ng’ombe wameuawa na watu wenye hasira
zaidi ya sabini , kwa kupigwa na kuchomwa moto katika kijiji cha
sheluhi wilayani iramba, baada ya kukutwa wakiwa wamewachinja ngo’mbe
hao.
Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo mwenye kiti wa kamati ya
ulinzi na usalama wa wilaya ya iramba ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo
Bwana Yahaya Nawanda amewataka wananchi wanapo wakamata wahalifu kuacha
vitendo vya kujichukulia hatua za kuwauwa kwa kufanya hivyo wanakuwa
hawalisaidii jeshi lapolisi.
kwaupande wake mama wa mmoja wa marehemu pamoja na mashuhuda
wamesema kitendo cha mauaji yaliyo fanywa na wananchi wenye hasira
,hawa kufanya jambo la busara kwani wange pelekwa kwenye vyombo vya
sheria.
Vitendo vya wananchi kuamua kuwauwa wahalifu katika wilaya ya
iramba vimekuwa vikishamiri jambo ambalo siyo sahihi kwani wamekuwa
wakipoteza ushahidi na kupatikana kwa wahalifu wengine.
- ITV
Post a Comment