Whatsapp wamewapunguzia sababu ya kujitetea wale wote wenye
tabia za kutojibu message kwa kisingizio kuwa hawakuziona hata kama
zilionesha tiki mbili kuashiaria zimefika. Sasa Whats App imeongeza
alama ya kuonesha kuwa ujumbe umesomwa na muda ambao umesomwa.

Kuanzia sasa ujumbe ambao tayari umepokelewa na kusomwa utakuwa
unaonesha tiki mbili za blue upande wa kulia chini kwenye simu ya
mtumaji, na uki bonyeza juu ya ujumbe huo itakuwa ikionesha muda ambao
ujumbe huo ulisomwa.

Kabla ya maboresho hayo kulikuwa na aina mbili tu za tiki, tiki moja
ya kijivu ilikua ikionesha ujumbe umetumwa, tiki mbili za kijivu
ziliashiria ujumbe umefika.

Upande wa messages za group, tiki mbili za blue zitakuwa zikionekana pindi tu watu wote kwenye group wakiusoma ujumbe.
Ili kuona mabadiliko hayo, mtumiaji wa Whatsapp anapaswa ku update app hiyo kwenye simu yake.
إرسال تعليق