BAO
pekee la kiungo Paul Ngway, dakika ya 52 jioni ya leo limeipa Kagera
Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga
SC ilimaliza mchezo huo pungufu, baada ya Nahodha wake, Nadir Haroub
‘Cannavaro’ kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80 na refa Abdallah
Kambuzi wa Shinyanga, baada ya kumpiga kichwa Rashid Mandawa wa Kagera.
Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Yanga SC walimtisha refa kiasi cha kutolewa uwanjani kwa msaada wa askari wa Polisi.
Kagera Sugar: Agathon
Anthony, Benjamin Asukile, Abubakar Mtiro, Erick Kyaruzi, George
Kavilla, Babu Ally, Julius Ambrose, Paul Maona, Rashid Mandawa, Atupele
Green na Adam Kingwande.
Yanga SC: Deo
Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson
Santos ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho. GPL
إرسال تعليق