Abomoa nyumba za majirani akitaka uchumba na winchi

MHOLANZI mmoja amesababisha hasarakubwa kwa majirani zake baada ya staili aliyotaka kuitumia  kuomba mkono wa ndoa kuvurugika.
Mholanzi huyo alipanga kuomba mkono wa ndoa kwa kuning’inia katika winchi.
Imeelezwa kuwa winchi hiyo ya katika gari haikuwa imeshikizwa salama barabarani wakati ilipojipindua na kupiga nyumba ya jirani na kusababisha nyumba nyingine 2 watu wake  kuokolewa.
Lengo la kujishusha mbele ya dirisha la chumba cha mchumba liligeuka dhahma lakini mke  pamoja na shida iliyotokea  amesema ndio na sasa wapo Paris kufurahia makubaliano yao.
Imeelezwa kuwa hasara kubwa zaidi ilitokea wakati wakijaribu kuiweka sawa winchi hiyo.
Wakazi wa majengo hayo waliondolewa lakini hakuna mtu ambaye ameumia katika shida hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post