Ofisa
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe ya
simu kwa msimu huu wa sikukuu ya Krismasi, ambapo itawawezesha wateja wa
Airtel kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya
bure vya muda wa maongezi, ujumbe mfupi na huduma ya intaneti. Kushoto
ni Meneja Masoko wa Bidhaa za Kisasa wa Airtel, Prisca Tembo.
Meneja
Masoko wa Bidhaa za Kisasa wa Airtel, Prisca Tembo (kushoto) na Ofisa
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde wakionyesha kwa waandishi wa
habari, baadhi ya simu za mkononi zilizo kwenye ofa kabambe ya simu kwa
msimu huu wa sikukuu ya Krismasi, baada ya kuzindua ofa hiyo, jijini Dar
es Salaam jana, ambapo itawawezesha wateja wa Airtel kununua simu za
kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya bure vya muda wa maongezi,
ujumbe mfupi na huduma ya intaneti.
Airtel
Tanzania imetangaza ofa kabambe inayoenda sambamba na kuwazawadia
wateja wake wakati wa msimu huu wa sikukuu, ofa hii iliyozinduliwa rasmi
leo itawawezesha wateja kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata
vifurushi vya bure vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet
Akiongea
wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa bidhaa za kisasa Bi Prisca
Tembo alisema” tunayofuraha kuzindua ofa hii ya msimu wa sikukuu na
kuwawezesha wateja wetu kununua simu kwaajili yao na kwaajili ya wale
wanaowapenda kwa bei nafuu zaidi sokoni.
Tembo
aliongeza kwa kusema “Ofa hii inaenda sambamba na dhamira yetu ya
kuendelea kutoa huduma bora huku tukiwawezesha wateja wetu kufaidika na
huduma na bidhaa zetu. Simu hizi za kisasa (yaani smart phone)
zinapatikana katika maduka yetu ya Airtel nchi nzima kwa gharama
kuanzia shilingi 125,000/= hadi 979,000/=. Mteja atakaponunua simu
hizi atapata na vifurushi vya muda wa maongezi, sms na internet vya
mwenzi mzima, ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu
Ofa
hii si ya kukosa, hivyo Tupenda kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia
ofa hii kwa kuwa wakwanza kununua simu ya aina wanayoipenda na kufurahia
huduma zetu na kuunganishwa kwenye huduma ya internet ya 3.75G .”
aliongeza Tembo
Kwa
upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” simu
tulizonazo kwenye ofa ni pamoja na iphone 6, simu za Huawei na Techno.
Simu hizi za kisasa ni rahisi kutumia na zitawapatia wateja wetu uzoefu
tofauti si kwa bei rahisi tu bali zimewezeshwa na techonologia ya 3G na
kuwawezesha kufurahi internet ya kasi.”
Natoa
wito kwa wateja kutembelea ofisi zetu na kunua simu na kuunganishwa na
huduma zetu nyingi ikiwemo Airtel yatosha, Airtel Money, huduma ya
internet na vifurushi vya OMG, Switch On pamoja na huduma yetu mpya ya
WiFi ya nyumbani tuliyoizindua hivi karibuni aliongeza Matinde.
إرسال تعليق