
Mkuu
wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akipata maelezo kutoka kwa
Dr.Anna Kichambati wa Redcross Tabora wakati wa sherehe za wiki ya
usalama barabarani mkoani Tabora.

Mkuu
wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akisalimiana na Afisa mfawidhi wa
Sumatra mkoa wa Tabora Bw.Joseph Michael wakati wa wiki ya usalama
barabarani mkoa wa Tabora.

Mmoja
kati ya maafisa wa polisi kikosi cha usalama barabarani Tabora mjini
akimuonesha mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila kifaa maalumu
kinachotumika kupima kiwango cha ulevi kwa madereva wazembe.

Kikosi cha zimamoto mkoa wa Tabora kikionesha vifaa vinavyotumika wakati wa uokoaji ajali zinapojitokeza.

Sherehe
za wiki ya usalama barabarani mkoa wa Tabora zilianza kwa maandamano
yaliyopita mitaa mbalimbali hadi viwanja vya mazoezi ya Jeshi la Polisi
Tabora ambapo wananchi walishiriki maandamano hayo.

Kamanda
wa Polisi mkoa wa Tabora kikosi cha usalama barabarani SSP Peter
Mnyandwa akitoa taarifa ya ongezeko la ajali za barabarani mkoani
Tabora ambapo zaidi ya watu 150 wamefariki dunia katika ajali 399 huku
watu 520 wamejeruhiwa katika ajali 185.

Mkuu
wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akihutubia katika sherehe hizo
za wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambapo mbali ya kusikitishwa na
taarifa ya ajali hizo lakini alisema kuwa asilimia 75 ya ajali hizo
zinatokana na makosa ya kibinadamu na hivyo kuzitaka mamlaka husika
kuchukua hatua ya kudhibiti kupunguza ajali hizo ikiwa ni pamoja na
kutotoa leseni kwa madereva ambao hawajapata mafunzo ya udereva
darasani.

Mkuu
wa mkoa wa Tabora Bw.Mwananzila akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti
mstaafu wa Kamati ya Usalama barabarani mkoa wa Tabora Bw.Moshi Abrahamu
maarufu Nkonkota.

Mkuu
wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akikabidhi cheti cha pongezi
kwa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya NBS kwa usafirishaji salama bila
kusababisha ajali kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja.
إرسال تعليق