ALEWA, ATANGAZA KUOLEWA NA DIAMOND BURE

http://4.bp.blogspot.com/-e54OdKpVqA8/Um8WySrvEvI/AAAAAAAAfzI/a9TzRkm1hSY/s640/IMG_0292.JPGKAMA kawaida, Ijumaa iliyopita mapaparazi wetu wanaotii amri ya bosi wao, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’, Musa Mateja ‘Tozi’, Shani Ramadhani ‘Mamaa Libeneke’ na Dustan Shekidele ‘Mkude Simba’ walisambaa kwenye viwanja tofautitofauti vya burudani huku wakiwasiliana moja kwa moja na mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya ofisi za gazeti hili, Bamaga–Mwenge, jijini Dar.
Mkuu akiwa ofisini kwenye kiti chake cha kuzunguka huku akiangalia TV, anabaini muda wa waandishi wake kumpa ripoti umefika na moja kwa moja anaanza kumpigia simu Shani Ramadhani ‘Mamaa Libeneke’.
Saa 4:01 usiku
ALEWA, ATANGAZA KUOLEWA NA DIAMOND BURE
Makao Makuu: Shani Ramadhani ‘Mamaa Libeneke’ haya kazi ni kwako, jismatifonishe basi utupe mahabari ya mujini.

Shani: Mkuu nipo maeneo ya Hongera Baa, naangalia watu wanavyosindikiza wikiendi zao.
Makao Makuu: Siyo uangalie tu, umebaini kitu gani hapo? Au unasindikiza wikiendi yako tu na wewe.
Shani: Hapana Mkuu wangu hapa ni kazi tu, kuna watu wamelewa mpaka wanatia aibu.
Makao Makuu: Kivipi?

Shani: Ule usemi unaosema wewe unakiona cha nini wenzio wanasema watakipata lini leo umethibitika hapa, kuna mdada anajinadi kuwa yuko tayari kuolewa na Diamond bure bila mahari na muda wowote, eti kisa Wema kamringia.
Makao Makuu: Duh! Anamfahamu vizuri Diamond au anaongea tu.
Shani: Anaonekana si yeye lakini nahisi ana mapenzi ya dhati kwa Diamond maana anasema siku akibahatika kuonana naye atamwambia ukweli kwa jinsi anavyoteseka juu yake.
Makao Makuu:  Hiyo kali ya mwaka, endelea na kazi ngoja nimcheki Shekidele.

Saa 5:12 usiku
AMFUMANIA MKEWE
Makao Makuu: Haloo...Mkude Simba, vipi hali ya hapo Mji kasoro Bahari?
Shekidele: Mkuu hapa Moro ni shwari.
Makao Makuu: Lete habari.

Shekidele:  Nilikuwa kwenye Ukumbi wa Glonency Nanenane kwenye shoo ya Malaika Band nikapata taarifa ya tukio la fumanizi maeneo ya Kihonda.
Makao Makuu: Enhee  uliliwahi tukio hilo?

Shekidele: Ah Mkuu kutoka Nanenane mpaka Kihonda kuna kaumbali kidogo, lakini nilivyofika tu karibu na gesti hiyo nimeshuhudia difenda ya polisi ikiondoka na wagoni pamoja na mwenye mke huku watu kibao wakiangalia.
Makao Makuu: Umefanikiwa kupata picha japo mbili tatu?
Shekidele: Nimepata picha za kuibiaibia naamini zitafaa, nilifanikiwa kuongea na baadhi ya mashuhuda walisema kuwa huyo mwanamke aliyefumaniwa na mume wake alikuwa na hawara yake ambaye inasadikika kuwa wanafanya kazi katika kampuni moja huko Dar.

Makao Makuu: Sasa ilikuwaje wakaenda Morogoro, Dar gesti zimejaa?
Shekidele: Siyo kwamba huko hakuna gesti, wamekimbilia huku ili kuondoa urahisi wa kufumaniwa.
Makao Makuu: Huyo mwenye mke ni hatari sijui alitumia njia gani kumnasa mke wake.

Shekidele: Inasemekana mwenye mke machale yalimcheza baada ya mkewe kumuomba ruhusa kuwa anakuja huku kusalimia ndugu zake akamkubalia, baada ya kumruhusu akaenda Kariakoo kununua baibui na nikabu na kisha kupanda basi alilopanda mkewe mpaka wanafika hapa jamaa anamfuatilia tu mpaka alipofanikiwa kumnasa.
Makao Makuu: Jamaa katumia akili ya kuzaliwa, ana hoja! Ngoja nimcheki Musa.
MATUMLA AWACHIMBA MKWARA WATU
Makao Makuu: Bila shaka kijana wangu utakuwa umeshaingia ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee kwenye Tuzo za Taswa si ndiyo?
Mateja: Kweli Mkuu nipo hapa na muda huu ndiyo msafara wa mgeni rasmi unaingia.
Makao Makuu: Mgeni rasmi?

Mateja: Mkuu tuzo hizi leo ziko chini ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Makao Makuu: Ooh basi vizuri nipe ripoti sasa tuzo zimeshaanza kutoka ama ipo vipi?
Mateja: Ndiyo Mkuu tuzo nazo tayari zimeanza na kuna mdada mmoja anaitwa Sheridah Boniface tayari ameshachukua mbili pia Erasto Nyoni naye katwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka (wanaume).
Makao Makuu: Vizuri sana kingine kilinachojiri hapo nini ukiachana na tuzo.

Mateja: Kuna tukio la kibabe kalionyesha bondia wa zamani, Rashid Matumla.
Makao Makuu: Tukio gani hilo tena?
Mateja: Mgeni rasmi kapewa nafasi ya kuzungumza machache juu ya tuzo hizi, wakati anazungumza kuna jamaa wamekaa karibu na meza ya Matumla wakijimiminia ‘kilaji’ chao sasa si wamejisahau wanapiga kelele kama wapo baa, jamaa kakasirika amewaambia wakiendelea atawatuliza kwa makonde.

Makao Makuu: Duuh hilo nalo neno maana ninavyomjua Matumla na asivyokuwa na mzaha, hakawii kweli kuwainukia kama vipi usicheze mbali na meza hiyo maana waweza pata tukio la maana muda wowote.
Mateja: Kweli Mkuu nitakujuza tu, tuendelee kuwasiliana.
Makao Makuu: Piga kazi, ukimaliza hapo waambie wenzako mkalale maana hata mimi macho mazito hapa!

Post a Comment

أحدث أقدم