Wananchi wa mtaa Msalala road wakiangalia shimo ambalo limesababisha kifo cha mgombea wao Bertha Chimanyi usiku wa kuamkia leo-picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita |
Bertha Chimanyi enzi za uhai wake-picha na Valence Robert-Malunde1 blog Geita |
Kumetokea
sintofahamu ama kwa lugha nyingine hali isiyo ya kawaida iliyowastua
wananchi wa mtaa wa Msalala Road mkoani Geita ,ya kuondokewa na mgombea
wa nafasi ya wajumbe wa serikali za mitaa viti maalumu kupitia chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bertha Nchimanyi (40) baada ya
kukutwa amekufa kisimani.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9:00 wakati mgombea
huyo alipotoka nje kuongea na simu yake ya mkononi.
Inaelezwa
kuwa marehemu alikuwa akisimamia zoezi la kuhesabu kura zake,na wakati
zoezi hilo likiendelea alitoka nje kuongea na simu na hakurudi tena.
"Martha
nilikuwa naye ilipofika majira ya saa 9 usiku wakati tunahesabu kura
,aliniambia anatoka mara moja nje lakini hakurudi tena “aliiambia
Malunde1 blog,mgombea wa nafasi ya mwenyekiti kupitia Chadema Elineema
Mafie.
Naye
wakala wa mgombea huyo Maselina Simbasana ambyae alisaini matokeo ya
marehemu huyo baada ya kuonekana hayupo,alisema marehemu alikuwa na
mtoto mdogo hivyo walivyomtafuta walidhani huenda alikwenda nyumbani
kunyonyesha mtoto wake.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema:
na kwamba, jeshi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini chazo cha tukio.
“Ni
kweli kuna tukio la mgombea wa chadema kutumbukia kisimani, kwa taarifa
tulizonazo inaelezwa alitoka nje kuongea na simu wakati anaongea
hakujua kama kuna kisima kirefu eneo alilokuwepo, alitumbukia na
kufariki dunia”.
Katibu wa Chadema Jimbo la Geita Mutta Robert alisema kuwa kifo cha mgombea huyo ni Mapenzi ya Mungu .
“Mgombea
wetu ameondoka na alikuwa ameshinda ,alikuwa mchapakazi mzuri
,tulimpenda zaidi lakini Mungu amempenda zaidi na yote tunamwachia
yeye”alisema Robert.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Post a Comment