Rapper Nikki Mbishi ameibuka na kudai kuwataka mashabiki wa
muziki wa Tanzania kuwaunga mkono wasanii wengine pia na sio Diamond au
wasanii wengine wachache wanaopewa kipaumbele zaidi.
Akizungumza kwenye kipindi cha Genge cha EFM leo, Nikki Mbishi
alisema wasanii wote wanahitaji kusaidiwa ili wawepo wengi wakubwa.
“Hadi leo hii unataka kuniambia kuna super star mmoja Diamond na
wengine wote ni washkaji zotu tu wa mitaani wanaoturusharusha tu
majukwaani sio mastaa, hawana hadhi ya kuwa mastaa, mimi mwenyewe
nikiwepo,? amehoji Mbishi.
“Kwa wenzetu nje, msanii anakuwa label anakuja anatoa ngoma moja
kesho yake staa, anaishi maisha mazuri, gari nzuri, anaendesha maisha
yake vizuri na anapewa ile heshima kuwa huyu kweli ni icon. Hauoni kama
itakuwa siku tukiwa na watu kama Diamond mia mbili Tanzania, na kwanini
ile dhana ya utumwa Nikki Mbishi hata akawa nominated kwenye tuzo za
Zanzibar, lakini nobody is going to pay attention kwa kum-support Nikki
Mbishi kwa sababu ni msanii pekee!
“Acha Nikki Mbishi hawa akina Peter Msechu wanakuwa nominated
sometimeS kwenye matuzo makubwa duniani lakini you will never hear watu
wakisema jamani msupport Dabo, Mtanzania anayetuwakilisha, why Diamond
only? Kwamba Diamond akiwa kwenye show basi ndo watu muache shughuli
zenu mum-support? Sio hatuwezi ku- create watu kama yeye wakawa mia
mbili tukiwa watu wote tunamwangalia huyo mmoja? Yule atakuja kupotea
naye kwenye game ina maana watanzania kutakuwa hakuna kitu. Kama
tulivyoshindwa kwenye soka hivyo hivyo na tutashindwa kwenye muziki na
sisi tunachokiweza ni Big Brother.”
Post a Comment