|
Basi la kampuni ya Mohammed Trans limepata ajali mbaya Igunga ambapo watu saba wanadaiwa kupoteza maisha katika eneo la Makomero wilayani Igunga, mkoani Tabora.
Inadaiwa
kuwa mbali na kuua pia abiria wengi wamejeruhiwa baada ya basi hilo la
Mohammed Trans kukatika 'steeering power' likaacha njia na kupinduka
huku kukiwa na taarifa zingine kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi
hilo kugonga shimo
|
Basi hilo limepinduka leo majira ya saa nane mchana, ambapo maiti na
majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Picha zote zikionyesha mandhari ya sehemu ajali hiyo ilipotokea.
Post a Comment