ANGALIA PICHA 7- AJALI YA BASI LA MOHAMED TRANS, LAUA NA KUJERUHI HUKO IGUNGA TABORA

Basi la kampuni ya Mohammed Trans limepata ajali mbaya Igunga ambapo watu saba wanadaiwa kupoteza  maisha katika  eneo la Makomero wilayani  Igunga, mkoani Tabora.



Inadaiwa kuwa mbali na kuua pia abiria wengi wamejeruhiwa baada ya basi hilo  la Mohammed Trans kukatika 'steeering power' likaacha njia na kupinduka huku kukiwa na taarifa zingine kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kugonga shimo 
  Basi hilo limepinduka leo majira ya saa nane mchana, ambapo maiti na majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.


Picha zote zikionyesha mandhari ya sehemu ajali hiyo ilipotokea.



Post a Comment

أحدث أقدم