Chaka Khan amshauri Rihanna ‘Una sauti nzuri si lazima uoneshe mwili wako’

Muimbaji mkongwe wa Marekani, Chaka Khan amedai kuwa Rihanna ana sauti ya kutosha kuuza muziki bila hata kutumia mwili wake kufanya hivyo.
rihanna-esquire-uk-3
Muimbaji huyo mwenye miaka 61 anaamini kuwa si muhimu kwa Rihanna na wasanii wengine kama Ariana Grande kuona ulazima wa kuvua nguo kwenye video zao za muziki au kwenye photoshoots ili kuuza nyimbo zao. Hata hivyo amesema anaelewa kwanini wanafanya hivyo kwakuwa biashara ya muziki imebadilika ukilinganisha na wakati wao.
headshot-blue-dress Chaka Khan
“Kitu kimoja kuhusu wasichana hawa ni kwamba hawahitaji kufanya hivyo vyote. Rihanna walau ana sauti nzuri na anaweza kuuza nyimbo bila kuonesha ngozi zao,” aliliambia jarida la Ahlan.
“Tatizo ni kuwa industry imebadilika tangu enzi zangu. Biashara iko tofauti sasa.”

Post a Comment

أحدث أقدم