Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)Cyprian Luhemeja.
Wamedai licha ya kuhimizwa kuchimba mitaro ili kuruhusu wataalamu kuwaunganishia maji wakazi wa Chekereni, ahadi hiyo haijatekelezwa kwa miaka mingi.
Mmoja wa wakazi hao, Chausiku Salim, alisema kuwa kutokana na adha hiyo, idadi kubwa ya wakazi wa kijiji hicho wanalazimika kutumia maji ya mto Weruweru kwa ajili ya matumizi ya nyumbani ikiwamo kupikia na kunywa licha ya kuelezwa maji hayo si salama kwa afya zao.
Mkazi mwingine, John Malya, alisema wanashangazwa na Mamlaka hiyo kuchelewa kuwaunganishia huduma hiyo kwa muda mrefu wakati wanaelewa kwamba wanaoathirika na adha hiyo ni akina mama na watoto ambao hutumia muda mwingi kuyafuata maji hayo mtoni.
Alisema zaidi ya miaka saba sasa, wamekuwa wakienda katika ofisi za Mamlaka hiyo na kupewa majibu yasiyoridhisha kutokana na kushindwa kutumiziwa ahadi hiyo.
Akizungumzia adha hiyo, Muelimishaji wa usafi na mazingira wa Kijiji cha Chekereni, Jamila Omari, aliiambia NIPASHE kwamba hali ya wakazi wa kijiji hicho kiafya ni mbaya, licha ya kutumia muda mwingi kumwelimisha kila mkazi kuchemsha maji ya kunywa lakini bado tatizo la magonjwa ya tumbo katika kijiji hicho ni kubwa.
Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi, Cyprian Luhemeja, alisema hakuna malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake na kuahidi kufuatilia tatizo hilo kwa kuzungumza na viongozi wa serikali ya kijiji hicho ili kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wananchi hao.
Hata hivyo, taarifa ya hali ya huduma ya majisafi ya Muwsa, ya mwezi Julai, 2013 hadi mwezi Oktoba mwaka huu, inainisha matarajio yake kufikia Juni 30, 2015, ni kupanua mtandao wa kilomita 40.65 katika sehemu mbalimbali za mji ambazo bado hazijafikiwa na mamlaka.
CHANZO:
NIPASHE

Post a Comment