
Kampuni
ya ndege ya fastjet, ambayo ni Kampuni yenye gharama nafuu kote Afrika,
imeadhimisha miaka miwili ya kutoa usafiri wa anga barani Africa.
Fastjet
ilianza biashara ya usafiri wa anga hapa Tanzania tarehe 29 Novemba
2012, ikifanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro na
Mwanza kupitia ndege yake aina ya A319.
Tangu
wakati huo, Fastjet imepanua wigo wa mtandao wake nchini Tanzania
pamoja na kuanzishwa kwa njia yake ya tatu kwenda Mbeya. Kwa sasa
safari za Kimataifa za ndege hii ni pamoja na safari ya Dar es Salaam
kwenda Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Lusaka nchini Zambia,
Harare nchini Zimbabwe na Entebbe nchini Uganda.
Hadi
sasa, ndege imeshasafirisha zaidi ya abiria 870,000 katika safari zake
8,200 ilizofanya zenye umbali wa takribani kilomita milioni 6.5 – ambapo
utendaji wake kwa ujumla umevutia kwa asilimia 90 kwa mwaka 2014 kwa
kuwa usafiri wenye uhakika na wa kuzingatia muda. Kampuni imejijengea
kuwa ni ya uhakika, kuaminika na ya usafiri wenye gharama nafuu.
Nauli
za Fastjet katika safari za ndani ya nchi hapa Tanzania zinaanzia dola
za kimarekani 20 kwa safari moja, na nauli za kimataifa gharama ni ndogo
kuanzia dola 50 kwa safari moja, zote ukiondoa kodi ya uwanja wa ndege
na kodi ya serikali. Nauli hizi nafuu zimeifanya kampuni hii kutajwa
kuwa ni yenye gharama nafuu kwa Afrika na ya tano kidunia kwenye unafuu
wa bei ukilinganisha na makampuni mengine kupitia tovuti ya makampuni
ya ndege, WhichAirline.com
Fasjet
inaamini unafuu wake wa bei unafanya safari za anga kupatikana kwa
wingi kwa Waafrika wengi zaidi. Usemi huu ulihakikiwa kupitia utafiti
uliofanywa na Fastjet muda mfupi baada ya uzinduzi wake, ambao
ulionyesha kuwa asilimia 38 ya abiria wake walikuwa wanasafiri kwa mara
yao ya kwanza ambapo kabla hawakuwa na uwezo wa kusafiri kwa anga.
“Usafiri
wa anga wenye gharama nafuu ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi katika
Afrika- hasa katika sekta ya biashara na utalii,” amesema Jimmy Kibati,
ambaye ni Meneja mkuu wa kampuni ya Fastjet kwa Afrika Mashariki. “Hata
kama kuna ndege zilizopo zinazounganisha majiji miwili, kwa kawaida
ndege huwa inahusisha angalau kituo kimoja cha kusimama. Hivyo, nauli
kubwa inayotozwa na mashirika ya ndege kwenye safari za njia hizi
huwatenga wananchi wengi kufurahia urahisi na uokoaji muda unaotokana na
faida ya kusafiri na ndege.”
Kulingana
na Kibati, Fasjet imepiga hatua kubwa katika miaka hii miwili, licha ya
changamoto ambazo kampuni imekuwa ikikabiliana nazo.
“Licha
ya changamoto kubwa za udhibiti tulizokutana nazo wakati tunaanza
upanuzi wa safari za kimataifa, serikali ya Tanzania imekuwa ikitutia
moyo sana, kwa sababu hiyo tunawashukuru sana,” aliongeza Kibati. “Hii
inatufanya tuwe na mtazamo chanya juu ya siku zijazo, pamoja na maoni
yetu kwamba ukuaji wa uchumi katika Tanzania utaendelea, ukiendeshwa na
tabaka la kati linaloibuka, na kuongezeka kwa viwango vya mapato ya
hiari, ukuaji mkubwa katika ujasiriamali na uboreshwaji wa miundo mbinu
ya uwekezaji.
Kibati
pia alitoa maoni juu ya umuhimu wa kuwa na kitovu cha usafiri wa anga
katika mji wa kibiashara wa Tanzania. “Dar es Salaam itaendelea kukua na
kuwa kitovu cha viwanda na biashara katika Afrika na dunia kwa ujumla,
hii inasababishwa na nafasi yake ya kuwa kama lango la Afrika Mashariki,
maendeleo ya mafuta na akiba ya gesi na kuwa na miundo mbinu bora ya
uwekezaji,”
Kuhusiana
na usafiri wa anga kwa bei nafuu katika bara zima, Kibati alielezea,
“Tunaamini kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuwa mfano wa ndege zenye
gharama nafuu katika Afrika. Tumedhamiria kufanya kazi pamoja na
serikali katika bara zima ili kukuza faida ya ushindani katika sekta ya
anga. Hii itasababisha nauli ziwe nafuu kwa abiria. “
Kampuni ya Fasjet inaendelea kupanuka katika bara la Afrika pamoja na hivi karibuni kutangaza kwamba operesheni take mpya.
إرسال تعليق