
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Sanato Mhenge
(kusshoto) akipokea mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano wa
kimataifa wa Tabia Nchi kutoka kwa mwenyekiti wa bodi wa Forum CC Euster
Kibona ofisini kwake jijini Dar es salaam.

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Naibu wake Ummy Ali
Mwalimu wakimsikiliza Meneja mwezeshaji wa Taasisi ya Forum CC Rebeca
Muna wakati wakipokea mapendekezo ya asasi za kiraia kuelekea mkutano wa
kimataifa wa Tabia Nchi unaoendelea kufanyika Lima nchini Peru.

Ujumbe
wa Forum CC ukiongozwa na Meneja mwezeshaji wake Rebeca Muna( kushoto),
katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
mazingira Binilith Mahenge(wapili kutoka kushoto) na Naibu Waziri wake
Ummy Mwalimu(katikati), pamoja na mwenyekiti wa bodi ya Forum CC Euster
Kibona (wa pili kutoka kulia) na ofisa maendeleo wa Forum CC Adam
Anthony. wakati wa makabidhiano ya mapendekezo ya asasi za kiraia
kuelekea mkutano mkuu wa kimataifa wa TabiaNchi.
Akiwasilisha
mapendekezo hayo mbele ya Waziri mwenye dhamana na Mazingira Mwenyekiti
wa bodi ya Forum CC Euster Kibona amesema serikali inapaswa kubainisha
mapendekezo ya kupunguza makali ya uharibifu wa mazingira kwa nchi
zilizoendelea. Pia nchi zilizoendelea zikubali kuwepo na makubaliano ya
kisheria na kuheshimu kanuni juu ya masuala yote ya mazingira.
Kibona
ametoa wito kwa viongozi wa dunia na Afrika kuwashirikisha wadau
wengine katika mchakato wa mikataba ya kimataifa ili kupunguza
manung’uniko ya kutoshirikishwa kwa wadau. Pia amesema nchi
zilizoendelea zinapaswa kutoa fedha ,teknolojia na kujenga uwezo juu ya
kukabiliana na janga la uharibifu wa mazingira.
إرسال تعليق